MISS EAST AFRICA 2012 TANZNIA YATANGAZA MREBO ATAKAYEIWAKIRISHA
Asili Yetu Tanzania.Copyright
Mrembo atakaewakilisha Tanzania katika mashindano ya mwaka
huu ya Miss East Africa JOCELYNE DIANA MARO (22) katika pozi.
MREMBO huyo alipatikana kufuatia mchakato ulioendeshwa na
kamati maalum ya kuratibu zoezi hilo kwa zaidi
ya miezi mitatu iliyopita na kuwashinda warembo wengine 148 waliojitokeza
kutaka kuiwakilisha Tanzania
katika mashindano ya Miss East Africa 2012
Jocelyne amehitimu shahada ya Business Economics mwezi wa
saba mwaka huu katika chuo kikuu cha Keele
University, Nchini
Uingereza
Maandalizi ya mashindano hayo yanaendelea vizuri na yapo
kwenye hatua za mwisho ikiwa ni pamoja na kukamilisha taratibu zote za BASATA
ili kufanikisha mashindano hayo yatakayofanyika tarehe 07 December, 2012 katika
ukumbi wa Mlimani City Jijini Dar es
salaam
Mashindano ya Miss East Africa mwaka huu tayari yameanza
kuvuta hisia za watu wengi barani Africa kufuatia kiwango cha juu cha warembo
wanaowania taji hilo.
Nchi zilizothibitisha kushiriki mashindano hayo ni wenyeji Tanzania, Kenya,
Uganda, Rwanda na Burundi. Nchi zingine zilizoalikwa
kushiriki ni pamoja na Ethiopia, Eritrea, Somalia, Djibouti, Southern Sudan,
Malawi, pamoja na visiwa vya Seychelles, Madagascar, Reunion, Comoros, na
Mauritius.
Mashindano ya Miss East Africa yanalenga kukuza ushirikiano
na kutangaza utamaduni wa Afrika Mashariki, pamoja na kutangaza utalii wa Tanzania kama
Nchi wenyeji wa mashindano hayo makubwa katika ukanda huu wa Afrika
Mashindano ya Miss East Africa yanamilikiwa na kuandaliwa na
kampuni ya Rena Events Ltd ya jijini Dar es salaam,.

No comments:
KARIBU UTOE MAONI YAKO HAPA