Header Ads

Breaking News
recent

JACK WOLPER ANYAKUA TAJI LA IJUMAA SEXIEST GIRL.

Asili Yetu Tanzania.Copyright

Jacqueline Wolper (kulia), akipokea cheti cha ushindi kutoka kwa DK. Cheni aliyekuwa jaji mkuu wa shindano hilo.
MSANII wa chimbo la filamu Bongo, Jacqueline Wolper Masawe, usiku wa kuamkia leo ameibuka kidedea kwenye shindano lililokuwa likiwashirikisha mastaa wa kike Bongo la Ijumaa Sexiest Girl ndani ya Ukumbi wa Dar Live Mbagala jijini Dar es Salaam.

Wolper amejizolea heshima lukuki na kitita cha sh. milioni 2 ikiwemo na ofa ya kulipiwa saluni kujiremba kwa mwaka mzima.

Usiku wa leo pia ndani ya ukumbi huo kulikuwa na burudani kibao kutoka kwa Ommy Dimpoz, Chidy Benz, Dogo Asley, TOT Taarab na michezo kibao ya watoto iliyosindikizwa na shindano la Mkali wa Mic.

 Wolper akiwa ameshikilia cheti muda mchache baada ya kutangazwa mshindi.

Wolper akiwa stejini na Dkt. Cheni.

No comments:

KARIBU UTOE MAONI YAKO HAPA

Powered by Blogger.