AIRTEL YAZINDUA HUDUMA YA KULIPIA KODI KWA WATEJA WAKE KUPITIA AIRTEL MONEY.
Asili Yetu Tanzania.Copyright
Mkurugenzi wa Biashara za Mashirika wa Airtel bi Irene
Madeje Mlola (Kulia)akifafanua jambo wakati wa uzinduzi wa Huduma
itakayowawezesha wateja waAirtel kulipa kodi ya mapato na Majengo kwa kupitia
Huduma ya Airtel Money,pichani katikati ni Mwakilishi wa Kamishina Mkuu wa
Mamlaka ya Mapato Tanzania bw Saleh Mshoro akiongea na kushoto ni Kaimu Mkurugenzi wa hudumana elimu kwa mlipa
kodi bwn Allan Kiula.
**Kulipia kodi ya mapato na majengo
**Airtel na TRA kuwezesha ukusanyaji na ongezeko la mapato
Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel inayotoa huduma za
mawasiliano yenye gharama nafuu zaidi na mtandao wenye wigo mpana leo imezindua
mwendelezo wa huduma za Airtel kwa kushirikiana na Mamlaka ya Mapato Tanzania
(TRA) kwa kuwawezesha wateja wake nchi nzima kulipia Kodi kupitia huduma ya
Airtel Money.
Hii imekuja wakati huduma za pesa kutumia simu zimekuwa
zikibadilisha huduma za kibiashara na kuongeza ufanisi.
Kwa kupitia huduma ya Airtel money na ushirika na Mamlaka ya
Mapato Tanzania Airtel wateja wa makampuni hayo wataweza kulipia kodi ya mapato
na majengo kupitia Airtel Money.
Akiongea wakati wa uzinduzi uliofanyika makao makuu ya
kampuni ya Airtel, Mkurugenzi wa Biashara za Mashirika bi Irene Madeje Mlola
alisema” Airtel imekuwa mstari wa mbele katika kuleta ufanisi na mapinduzi
katika sekta ya mawasiliano nchini.
Leo tuna furaha kushirikiana na Mamlaka ya Mapato Tanzania
(TRA) kwa kuwezesha wateja wake kulipa kodi kwa kupitia huduma ya
Airtel Money.
Airtel money ni huduma iliyotengezwa kukithi mahitaji ya
wateja wetu na hii ni hatua nyingine muhimu kwa Airtel kutumia miundo mbinu
tuliyonayo na TRA katika kuhakikisha wanaboresha huduma zao. Sasa walipaji wa
kodi wadogo na wakubwa wanalipia kodi zao kwa urahisi wakiwa katika biashara
zao na nyumbani”
“Mpaka sasa takribani nusu ya wateja wa Airtel wamejiunga na
kutumia hudumaya Airtel money, huduma iliyo rahisi, iliyojitosheleza, salama na
nyenye kutoa nafasi kufanya miamala mbalimbali ikiwemo malipo ya bidhaa
mbalimbali.
Kwa kupitia huduma ya Airtel money inayotoa huduma nyingi
zaidi ya kutuma pesa tumeona maisha ya watanzania wengi yakibadilika kila siku
na biashara zao kuwa na ufanisi zaidi aliongeza Madeje.”
Kwa upande wake Kamishina Msaidizi Mkuu wa Mamlaka ya Mapato
Tanzania bw Rished Bade alisema” Tunayofuraha kuzindua huduma yenye kutumia
mfumo wa teknolojia ya malipo ya uhakika na salama kwa wateja wetu nchi
nzima.****
Uzinduzi wa leo ni udihirisho wa juhudi za Mamlaka katika
kuongeza uboreshaji katika huduma za malipo ya kodi na ukusanyaji wa mapato.
Tunategemea kwa kupitia huduma ya Airtel Money kutawezesha
ulipaji wa kodi kwa wakati na kuwahamasisha watanzania wengi zaidi kulipia kodi
zao za mapato na majengo. TUnategemea kuona ongezeko kubwa la wafanya biashara
wadogo na wakati ambao leo hii wanalipia malipo ya kodi kwa kupitia maofisi na
vituo mbalimbali vya kodi nchi nzima. ****
Akiongelea kuhusu njia ya kulipia kodi hizo kwa njia ya simu
Meneja Uendeshaji Airtel Money Asupya Naligingwa alieleza”Kulipia kodi ya
majengo au mapato mteja wa Airtel atatakiwa kupiga namba **150*60#*
kisha****
1. Atachagua
Lugha****
2. Atachagu malipo
ya bili ****
3. Lipa Bili****
4. Atachagu “JIna
la fumbo” *MAJENGO” *****
5. Ingiza kiasi cha
fedha unachotaka kulipia****
6. Ingiza neno la
siri****
7. Ingiza namba ya
akaunti ya Mamlaka ya Mapato (TRA) kisha bonyeza OK
na utapokea
meseji(SMS)itakayothibitisha malipo yako ”
Huduma ya Airtel Money service inayopatikana kwa kupiga **150*60# * inawawezesha wateja kulipia
huduma mbalimbali zikiwepo kama vile za kulipia bili za maji na umeme,bidhaa na
huduma mbalimbali kama vile bima,kununua
muda wa
maongezi,miamala ya huduma za kibenkiikiwemo kuweka na
kupokea kutoa na vile vile kulipia huduma nyingine nyingi.
Airtel Money ni huduma inayopatikana masaa 24, siku 7 za
wiki kutoka katika simu na ni salama ya uhakika na rahisi kutumia.
Kinachohitajika ni kitambulisho na usajili wa simu yako ili kuweza kupata
huduma hii katika maduka na mawakala wote waliopo nchi nzima.
No comments:
KARIBU UTOE MAONI YAKO HAPA