ASILI YETU BLOG: WAKE WA MFALME MSWATI WACHAPWA VIBOKO HADHARANI.
Asili Yetu © All rights reserved
Mfalme Mswati akiwa na baadhi ya wake wake.
TANGU Waziri wa Haki wa Swaziland, Ndumiso Mamba, anaswe
kitandani anavunja amri ya sita na mke wa Mfalme wa nchi hiyo, Makhosetive
Dlamini ‘Mfalme Mswati III’, hali ni mbaya kwa wake wa kiongozi huyo.
Mamba, alinaswa kwenye kitanda cha mke wa 13 wa mfalme huyo,
Nothando Dube na tangu wakati huo, walinzi wa Mfalme Mswati, wamepewa madaraka
makubwa ikiwemo kuwacharaza bakora hata barabarani na mbele za watu.
Inaelezwa kwamba wake wa Mfalme Mswati wanafungiwa ndani
kama kuku, inapotokea wanakwenda sehemu wanakuwa chini ya ulinzi mkali.
Ripoti zinasema kuwa endapo barabarani mke wa mfalme
atachepuka kwenda hata msalani bila taarifa au atasalimiana na mtu ambaye
walinzi wanamjua, hata kama ni ndugu yake, mwanamke husika hucharazwa bakora
kama ng’ombe.
“Ukiwa mke wa Mfalme Mswati ni mateso makubwa. Unavyoishi
haina tofauti na ng’ombe anavyochungwa. Ukiwa unatembea barabarani unatakiwa
ufuate uelekeo anaotaka bodigadi, ukikosea kidogo unachapwa bakora na vIrungu.
“Mambo yalikuwa
mabaya lakini sasa ni mabaya mno. Kwa sasa nataka kutoka lakini mfalme hataki
kuruhusu niondoke. Nipo kama mfungwa, saa 24 nachungwa, sina uhuru hata
kidogo,” alisema Nothando.
Mwanaharakati wa demokrasia anayepingana na mtindo wa maisha
ya Mfalme Mswati, Lucky Lukhele, aliwahi kuwaambia waandishi wa habari kwamba
siyo Nothando tu, wake wake wote wa kiongozi huyo wanaishi katika mazingira
magumu afadhali ya wafungwa.
“Kuna mke mmoja wa mfalme alikutwa getini na walinzi, tena
getini kwenyewe kwa ndani halafu geti lilikuwa limefungwa na funguo wanazo
walinzi. Ajabu ni kwamba walinzi walipomkuta pale hawakuuliza mara mbili,
walimpiga na kumuumiza mno,” alisema Lukhele bila kutaja jina la mke huyo wa
mfalme.
Kwa upande mwingine, inaelezwa kuwa mtindo wa maisha ya
Mfalme Mswati na wakeze, umesababisha mpaka sasa akimbiwe na wanawake watatu.
Mke wa sita wa mfalme huyo, Angela “LaGija” Dlamini, ndiye
anatajwa kuwa mwanamke wa hivi karibuni zaidi kuondoka katika himaya ya mfalme
huyo.
Mke wa 12 wa mfalme, Inkhosikati LaDube, alitimuliwa Desemba
mwaka jana kwa kile kilichobainishwa kwamba aligombana na bodigadi wake.
Taasisi ya Swaziland Solidarity Network ilieleza kwamba
Dlamini, alikimbia makazi ya mfalme baada ya kuwa kwenye mateso kwa miaka kadhaa.
Dlamini, aliaga anakwenda kuwasalimia wazazi wake kwenye Mji
wa Hhohho, lakini aliporuhusiwa alitimka jumla.
Mfalme Mswati pamoja na tabia ya kupenda kuoa mabikra,
vilevile anatuhumiwa kujilimbikizia utajiri wa kutisha, hivi karibuni Jarida la
Forbes lilimtaja kwamba anamiliki utajiri wenye thamani ya zaidi ya dola
milioni 200 (shilingi bilioni 300).

No comments:
KARIBU UTOE MAONI YAKO HAPA