MCHUNGAJI MTIKILA ASHINDA KESI, MENGINE YAIBUKA UPYA.
Asili Yetu © All rights reserved
MWENYEKITI wa Chama cha Democratic Party (DP), Mchungaji
Christopher Mtikila, ameshinda kesi ya uchochezi iliyokuwa inamkabili.
Inadaiwa kuwa Oktoba 21 mwaka jana katika maeneo ya Shirika la Nyumba la Taifa (NHC),
Ilala, jijini Dar es Salaam Mchungaji Mtikila alitoa maneno ya uchochezi,
dharau na kujenga chuki dhidi ya Serikali na Rais.
Akizungumza na mtandao huu baada ya kushinda kesi hiyo,
Mtikila amesema "Ushindi huu niliutarajia maana hata asubuhi kabla ya kuja
mahakamani niliongea na Yesu na sasa amenijibu".
Mara baada ya kushinda kesi hiyo lilizuka timbwili lingine
baada ya mtu mmoja kujitokeza akiwa na RB (Report Book) akimtuhumu Mchungaji
Mtikila kuwa alimtishia kumuua na ni mwizi wa viwanja. Baada ya kutaka
kukamatwa na polisi mmoja aliyekuwa na cheo cha Koplo, Mchungaji alikataa kwa
madai kuwa yeye ni kiongozi wa kitaifa hivyo hawezi kukamatwa na polisi mwenye
cheo cha Koplo, labda polisi mwenye cheo cha SSP (Senior Superintendent of
Police). Kwa kauli hiyo polisi alishindwa kumtia nguvuni.
No comments:
KARIBU UTOE MAONI YAKO HAPA