Header Ads

Breaking News
recent

SIMU ZA MKONONI NCHINI TANZANIA NA MADHARA YAKE.

Asili Yetu © All rights reserved


Simu ni kifaa muhimu sana cha mawasiliano katika jamii, lakini mara kitumikapo vibaya huleta madhara makubwa sana katika jamii yoyote ile. Tanzania ni nchi miongoni za mbele kabisa katika kuwa na idadi kubwa ya watumiaji wa simu za kiganjani ambapo jarida la "Business Monitor International liliandika kuwa huenda kufikia mwaka 2015 watumiaji wa simu za kiganjani Tanzania watafikia idadi ya 36.6 millioni.

Simu za kiganjani nchini Tanzania zilianza miaka ya 90 ambapo baadhi ya watanzania wachache wenye uwezo ndio walioweza kumiliki simu hizo.Lakini kuongezeka kwa utandawazi na kupanuka uchumi wa nchi, idadi ya wamiliki wa simu za mkononi iliongezeka huku Serikali ikiruhusu makampuni mbali mbali ya kigeni kuwekeza hapa nchini katika simu za mikononi kama vile mobitel, Buzz na nyinginezo za wakati huo.

Hadi kufikia sasa kuna kampuni takribani saba za simu za mkononi hapa nchini ambazo ni Vodacom, Airtel, Tigo, Zantel, TTCL, Sasatel na Benson Informatics. Kufikia mwezi desemba, 2011, mamlaka ya mawasiliano Tanzania ilibainisha kuwa na watumiaji wa simu za mkononi wapatao milioni 20.983.

MADHARA YATOKANAYO NA SIMU ZA MKONONI

- Uongo kuongezeka kwa kiasi kikubwa katika jamii Mfano; unampigia mtu simu anakwambia niko mbeya, kwa wakati yuko nyumba ya pili.
- Maovu ya uharifu kuongezeka, huku simu ikitumika kupanga mbinu mbali mbali za uharifu.
- Ndoa kuvunjika na kuongezeka kwa vitendo vya ngono.
-Vifo, ikiwa ni pamoja na kuripukiwa na simu wakati wa maongezi.
-Kupiga simu bila mpangilio kunasababisha kupunguza kipato cha mtumiaji.
-Utumiaji internet katika simu kuchati (facebook, twitter) muda wote bila mpangilio wa masaa maalum ya matumizi.

No comments:

KARIBU UTOE MAONI YAKO HAPA

Powered by Blogger.