REDD'S MISS TEMEKE KUJINYAKULIA KITITA CHA MILIONI 1.5 KESHO.
Asili Yetu © All rights reserved
Warembo wa Redd's Miss Tanzania
MALKIA atakayetwaa taji la Redd’s Miss Temeke 2012 katika
shindano linalofanyika Ijumaa Sept 21 katika ukumbi wa PTA(SabaSaba Hall),
atajinyakulia zawadi zinazofikia milioni 1.5 sanjari na tiketi ya moja kwa moja
kushiriki shindano la Redd’s Miss Tanzania baadaye mwaka huu.
Katika mlolongo huo wa zawadi, mshindi wa kwanza
atajinyakulia fedha taslim Sh. Milioni 1. Mshindi wa pili atajinyakulia fedha
taslim Sh.laki nane wakati mshindi wa tatu atapata Sh. Laki saba na washindi
wote watatu kila mmoja atajipatia nguo ya kutokea jioni sanjari na viatu,
vikiwa na thamani ya kila mmoja Sh. Laki
5.
Duka la kisasa la Mariedo Boutique itatoa gauni la
Sh.350,000 na kiatu cha Sh 150,000 kila mmoja kwa washindi hao watatu wa kwanza
watakaoshinda. Mbali ya washindi hao, mshindi wa nne atajinyakulia kitita cha
Sh. 400,000 ambapomshindi wa tano ataondoka na Sh 300,000 wakati warembo
wengine wote watakaosalia kila mmoja atapata Sh.200.000.
Ikiwa ni funga dimba ya mashindano ya urembo ya kanda
nchini, shindano hilo litanogeshwa na wasanii wanaong’ara katika luninga, Mpoki
wa kundi la Komed Original na Steve Nyerere ambaye mbali ya kuigiza sauti za
watu mbalimbali, pia ametoa filamu kadhaa kwa siku za hivi karibuni.
Mbali ya wasanii hao, bendi ya Mashujaa Musica,yenye
wanamuziki nguli kama Charles Baba, MCD, Ferguson, Ali Akida sanjari na
wanennguaji kama Lilian Internet na wengineo pia itanogesha usiku huo.
Taji la Redd’s Miss Temeke, linashikiliwa na mrembo Husna
Twalib. Warembo wa Miss Temeke wamekuwa wakijifua kwa wiki tatu sasa chini ya
ukufunzi wa Leyla Bhanji, ambaye amekuwa akisaidiwa pia na warembo wa miaka ya
nyuma wa Miss Temeke akiwemo, Regina Mosha(20020, Hawa Ismail(2003), washiriki
wa mwaka jana Joyce Maweda, Mwajabu Juma, Cynthia Kimasha na katika shoo
wamekuwa na Dickson Daud kutoka kundi la THT.
Shoo ya ufunguzi itakuwa tofauti kabisa na shoo nyingine
yeyote iliyowahi kuyanyika nchini, kwani imezingatia zaidi urembo na nini
msichana anatakiwa kufanya na si unenguaji tu. Warembo 15 wanatoka katika
vitongoji vya Kigamboni, Kurasini na Chang’ombe ambapo kila sehemu wametoka
warembo watano ambapo washindi watatu wa kwanza watapata fursa ya moja kwa moja
kushiriki Redds Miss Tanzania 2012.
Warembo hao ni Agness Goodluck, Angela Gasper, Flaviana
Maeda,Edna Sylvester, Catherine Masumbigana, Khadija Kombo, Neema Doreen, Flora
Kazungu, Lilian Joseph, Elizabeth Peter, Elizabeth Boniphace, Jesca Haule,
Zulfa Bundala, Mariam Ntakisivya na Esther Albert.
Mbali ya Redd’s, Miss Temeke 2012 pia imedhaminiwa na City
Sports Lounge, Jambo Leo, Mariedo Boutique, Global Publishers, Dodoma Wine,
Push Mobile, Mariedo Boutique, 100.5 Times FM, Kitwe General Traders, Fredito
Entertainment, katejoshy.blogsport.com na 88.4 Cloud’s FM.
Temeke imewahi kutwaa taji la Miss Tanzania mara tatu,
kupitia warembo Happiness Sosthenes Magesse aka Millen mwaka 2001, Sylvia Remmy
Baham mwaka 2003 na Genevieve Mpangala. Lakini pia imetoa warembo waliowahi
kushika nafasi ya pili na tano bora katika Miss Tanzania kama Jokate Mwegelo,
Irene Uwoya, Irene Kiwia, Queen David, Cecylia Assey, Sabrina Slim, Miriam
Odemba, Ediltruda Kalikawe na Asela Magaka.

No comments:
KARIBU UTOE MAONI YAKO HAPA