ASILI YETU BLOG: MWALIMU MKUU WA SHULE YA SEKONDARI YA ILBORU ARUSHA, ASIMAMISHWA KAZI.
Asili Yetu © All rights reserved
SERIKALI imemsimamisha kazi, Mwalimu Mkuu wa Shule ya
Sekondari ya Ilboru, Jovinus Mutabuzi, kufuatia madai ya tuhuma
mbalimbali za fedhana matumizi mabaya ya madaraka yaliyosababisha
wanafunzi kuandamana hadi ofisi ya Mkuu wa Mkoa wakishinikiza ang’olewe kutokana
na tuhuma za ulaji fedha na matumizi mabaya ya madaraka.
Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na
Serikali za Mitaa, anayeshughulikia Elimu, Kasimu Majaliwa, alitangaza
uamuzi huojana baada ya
kusikiliza madai ya wanafunzi katika mkutano wa hadhara uliofanyika shuleni hapo.
Pamoja na kusimamishwa kazi, Naibu Waziri Majaliwa, amemteua
Mwalimu Mkuu Msaidizi wa shule hiyo ya wanafunzi wenye vipaji
maalum, iliyopo wilayani Arumeru, mkoani Arusha, Lorna Nteles, kukaimu
nafasi ya Mwalimu Mkuu.
Katika hatua nyingine, Majaliwa, amemuagiza Mkurugenzi
Mtendaji wa Halmashauri ya Arusha, Halfa Hida, kuteua mkaguzi wa ndani
kufanya uchunguzi wa tuhuma zinazomkabili Mutabuzi, ikiwemo ya
kutumia stakabadhi bandia anazodaiwa kuhalalisha malipo ya
wanafunzi.
Katika mkutano wake wa hadhara na wanafunzi hao, Majaliwa,
alibaini kuwa hoja zao ikiwemo ya matumizi mabaya ya fedha kiasi cha
Sh.milioni 800 kuziingiza kwenye Chama cha Kuweka na Kukopa
(SACCOS) ambapo alikuwa akizikopesha kwa riba kwa walimu na watumishi
wa shule hiyo.
Jumatatu wiki hii, wanafunzi wa shule hiyo waliandamana hadi
ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Magesa Mulongo, kwa lengo la
kushinikiza kung’olewa kwa mkuu huyo, ambapo pamoja na mambo mengine
walidai kuwa ameshiriki kuifanya shule hiyo kudorora kitaaluma na
kuwadhalilisha wanafunzi kwa kuwaita mashoga.
Mkuu wa Mkoa Magesa aliwasihi wanafunzi hao kurejea shuleni
na kuendelea na masomo wakati suala lao likishughulikiwa, hata
hivyo, baaada ya kurudi shuleni walianzaisha mgomo wa kutoingia
darasani ikiwemo kutokula chakula cha shule hiyo.
Hatua hiyo, ilimlazimu Naibu Waziri, kufika shuleni hapo
na kuwasikiliza wanafunzi hao, ambapo kabla ya kufanya mkutano alitembelea maeneo yote yanayolalamikiwa na wanafunzi hao
ikiwemo, jiko la chakula, mabweni pamoja na choo cha matundu mawili
kinachodai
kujengwa kwa Sh. milioni 25.
Akizungumza katika mkutano wa hadhara shuleni hapo, Majaliwa
aliwasihi wanafunzi hao kutovunja sheria kwa kuitisha migomo na
maandamano yasiyo rasmi huku akimtaka makamu wa shule hiyo kusimamia
nidhamu kwa wanafunzi hao.
Naibu waziri akiwa ameandamana na askari wa kikosi cha kutuliza ghasia waliokuwa na mabomu na silaha za moto, alilazimika
kutumia saa zaidi ya tano kutoa ufafanuzi wa madai ya wanafunzi hao
ambao muda wote walionyesha kumsikiliza kwa makini huku hoja yao kubwa
wakidai hawamtaki mkuu huyo.
Hata hivyo, Mjaliwa
alikerwa na mabango aliyoyakuta yamebandikwa kwenye kuta katika majengo yote ya shule yakiwa na ujumbe
mbalimbaliwa kumpinga Mwalimu Mutabuzi huku baadhi yake yakiwa
yamechorwa vikaragosi vinavyomfananisha utawala wa mkuu huyo na ule wa marehemu Nduli Idd Amini dada wa Uganda.
Pamoja na kuwasihi kuwa wawe wavumilivu wakati hatua zaidi zikichukuliwa lakini walipaza sauti wakidai kuwa hawapo
tayari kuingia darasani bila kuondolewa kwa mkuu wao hali iliyomlazimu
Naibu Waziri kutamka kuwa amemsimamisha kupisha uchunguzi wa tuhuma hizo,
hali iliyoamsha shangwe na nderemo kwa wanafunzi hao.
Naibu waziri amepiga marufuku michango isiyo na tija
mashuleni, matumizi ya simu za mkononi kwa wanafunzi, adhabu za malipo
ya fedha, matumizi ya M-Pesa mashuleni pamoja na kuziagiza bodi za
shule kutatua matatizo ya wanafunzi pale yanapoibuka kabla ya kuleta
madhara
No comments:
KARIBU UTOE MAONI YAKO HAPA