Asili Yetu © All rights reserved
Mjane wa marehemu Daudi Mwangosi mwandishi wa habari aliyeuwawa mkoani Iringa, akiwa katika majonzi makubwa ya kumpoteza kipenzi chake. R.I.P Daudi.
Kufuatia kifo cha mwandishi wa habari na m/kiti wa chama cha waandishi wa habari mkoani iringa ipc marehemu David Mwangosi chama hicho mkoa kikieleza kushauriana na jukwaa la wahariri nchini kimetangaza kususia kazi za jeshi la polisi mkoani humo hadi watakapokuwa wametoa taarifa za kweli dhidi ya wahusika na kuacha propaganda juu ya tukio hilo.
KATIKA MTANDAO WA FACEBOOK NAO HAUKUSITA KUNENA HAYA.
Polisi wa Tanzania sikieni!
Mmepewa jukumu kubwa sana na taifa hili la kulinda usalama wa raia wake. Lakini kinyume chake, nyinyi mmekua mstari wa mbele katika kunyanyasa na hata kuwatoa uhai raia wa Jamuhuri hii ya Tanganyika.
Angalieni yatima mliowaongeza, kwa kuwaua wazazi wao, angalia wajane wanaolia kwa ajili yenu, angalieni walemavu mliowasababisha na angalieni wataalamu mliowaangamiza kwa fitina na kesi za kuwasingizia.
Hivi nyinyi mnamwabudu Mungu gani?!
Kumbukeni na nyinyi ni binadamu, iko cku mtakufa kama hawa mnaowakatisha maisha kila kukicha.
POLISI WA TANZANIA MUOGOPENI MUNGU!!
No comments:
KARIBU UTOE MAONI YAKO HAPA