Asili Yetu © All rights reserved
RIHANNA & OPRAH WINFREY
Huenda mwanadada Rihanna akawa amejeruhiwa kimwili na kihisia katika kuachana na Shalo balo Chris Brown, lakini hii haimaanishi kuwa amefuta kumbu kumbu zote kwa Chris Brown. Katika video mpya kutoka sehemu ya pili ya kipindi cha Oprah kinachofuata, nyota wa R&B Rihanna amemwambia Oprah Winfrey kuwa wakati mwingine huwa anamkosa (misses) sana Xboyfriend wake 'Chris Brown' " namkumbuka kwa vitu kibao vizuri kama, ziara tulizoenda, tuwapo vyumbani katika hoteli, muziki, nyimbo na vitu kibao. Namkosa mara kwa mara.
Rihanna alipoulizwa kuwa nini anachohitaji zaidi kutoka kwa mwanaume? Alifunguka....""Nataka mtu anipendaye nilivyo mimi, maadili yangu, lakini wanatakiwa kujua thamani ya thamani yangu. Watajua thamani yangu endapo watatambua uthamani wangu kwao". Aliendelea kufunguka " Nahitaji watu waniheshimu, pia hakuna kitu ninachokipenda kama kucheka, lakini zaidi nahitaji ushirika katika uharifu ( All I want is a partner in crime." ).
Katika mahojiano haya yatakayorushwa rasmi siku ya Jumapili Augost 19 / 2012ndani ya kituo cha luninga cha 'OWN', Oprah ataandamana na Rihanna hadi Barbados mji aliozaliwa Rihanna, na huko ndio mpango mzima wa kipindi utakapotedeka. Cheki kipande kimojawapo cha mahojiano hayo hapo chini.

No comments:
KARIBU UTOE MAONI YAKO HAPA