Asili Yetu © All rights reserved
 |
| Hapa ni mlango wa kuingia ndani ya maonyesho 19 ya wakulima ya nane nane kanda ya kaskazini, ambapo kauli mbiu ni "KILIMO KWANZA". |
 |
| Hili ni banda la Benki kuu ya Tanzania, hapa tumepata kupewa maelekezo mafupi jinsi ya kutambua pesa bandia (noti) na maswala ya kibenki pamoja na ripoti ya mwisho wa mwaka wa 2011 - 2012 katika uchumi wetu. |
 |
| Hapa ni mmoja wa watoa mafunzo kwa wananchi waliotembelea banda hili la benk ya taifa, akitoa maelekezo ya jinsi ya kutambua noti bandia na halali. |
 |
| Hili ni banda la shirika la posta Tanzania na hapa wanatoa maelekezo yote kuhusiana na shirika hilo pamoja na jinsi wasafirishavyo barua na mizigo mbali mbali. |
 |
| Hili ni banda la mpango wa kudhibiti UKIMWI. |
 |
| Hili ni banda maalum kabisa kwa kutoa elimu kwa watu wote jinsi ya kutumia kinga, uzazi wa mpango na kutumia kondom ya kike maarufu kama LADY PEPETA. |
 |
| Banda la chuo cha ufundi Arusha. |
 |
| Hapa ni momoja wa wahusika katika banda la mapato (TRA) akitoa maelezo kwa watu wanaolitembelea banda hilo. |
 |
| Hili ni banda la mali ya asili na utalii, hapa wanatoa maelezo mbali mbali ya hifadhi zote za taifa pamoja na ugunduzi wa vitu na sehemu za kihistoria. |
 |
| Watu mbali mbali waliohudhulia banda hili wakipewa maelezo kuhusu wanyama pori. |
 |
| Hili ni banda la polisi, kama umebahatika kufika hapa basi, utakuwa umepewa elimu mbadala kuhusu sheria za uharifu pamoja na faida ya polisi jamii. |
 |
| Huyu ni mkuu wa kitengo cha polisi jamii kwa wanawake yani (Tanzania Polisi Female Network) Merry Lugola akitoa ufafanuzi wa jinsi wananchi wanavyohusika katika ulinzi shirikishi. Lugola amesema wananchi wanapaswa kujifunza jinsi ya kubaini, kuzuia na kupambana na uharifu. |
 |
| TAHA - Ni Tanzania Horticultural Association - ni taasisi inayoshughulikia maswala mbali mbali ya kibiashara ya wazalishaji, wasafirishaji, wasindikaji pamoja na watoa huduma mbali mbali katika sekta ya horticultural. |
 |
| Banda la Kanisa la Kiinjiri la Kikristo Tanzania idara ya wanawake na watoto, hapa kuna vitu kibao pamoja na vile vya kiasili. |
 |
| Hizi ni baadhi tu ya kazi wazifanyazo wanawake hawa na wengine katika idara hii. |
No comments:
KARIBU UTOE MAONI YAKO HAPA