All rights reserved to Asili Yetu.
SAFARIE (Ego Omalicha)
Mwanadada huyu aliyekuwa akiitwa "Ego" ameamua kufunguka kuhusu sababu iliyofanya abadili jina la kisanii. Mwiimbaji huyu ambaye kwa sasa anaitwa "Safarie" amesema kuwa ameamua kubadili jina kutokana kuwa wamekuwa wakina "Ego" wawili katika game la muziki kwa muda sasa, kitu ambacho kimekuwa kinawachanganaya mashabiki wake "kwamfano "Ego" mwenzangu amechaguliwa katika tuzo za muziki, watu wanaanza kunipigia wakinipongeza, kitu ambacho kinanitaka nianze kumuelezea kila mmoja kuwa sio "Ego" mimi"
"Pia hata tukirekodi wimbo unakuwa ni utata mtupu, na hii inanirudisha nyuma mimi kwasababu nimekuwa nikigawana jina na mtu mwingine, inawa alikuwepo kabla yangu.Nimeamua kuwa najina jipya na mtindo wangu mpya".
No comments:
KARIBU UTOE MAONI YAKO HAPA