Asili Yetu © All rights reserved
Kuna aina mbali mbali za mmomonyoko wa udongo, kama vile mmomonyoko unaosababishwa na binadamu, Upepo, brafu, pwani na maji.
Mabadiliko kutokana na kazi za kibinadamu husababisha mara nyingi mmomonyoko wa ghafla unaoshtusha na kuleta hasara. Mfano ni kukata miti hasa kwenye mitelemko ya milima au kulima milimani. Kazi hizi zinapunguza au kuondoa kabisa funiko la mimea na kuacha udongo bila hifadhi. Maji ya mvua na upepo hazina vizuizi tena.
Matokeo yake ni mafuriko ya ghafla kwa sababu wakati wa mvua maji huteremka haraka na mara moja yakichimba mifereji, kuharibu nyumba, kuua watu na kuondoa ardhi yenye rutuba kwenye mashamba.
Njia nyingine ni mmomonyoko kutokana na kuzidi kwa mifugo. Kazi ya kukanyaga kwa miguu mingi hasa kwenye njia zilezile zinazotumika kuzunguka kati ya boma, maji na sokoni kumeleta uharibifu mwingi.Kwato za mifugo kama ng'ombe, mbuzi, punda na wanyama wengine wafugwao huathiri udongo mara wanapokanyaga mara kwa mara na hivyo hufanya udongo huo kuwa rahisi kusombwa na wakala wa mmomonyoko, kama vile maji, barafu na upepo.
Baadhi ya watu wakishuhudia mgodi unaochimbwa mawe ukiporomoka hadi kutoa moshi hivi karibuni huko Arusha.


No comments:
KARIBU UTOE MAONI YAKO HAPA