Asili Yetu © All rights reserved
Hakuna anayependa hata siku moja asione kinachoendelea hapa duniani, lakini kutokana na mambo mbali mbali ya kimaisha na hata kuzaliwa, hujikuta mtu anakuwa kipofu katika maisha yake yote. Ni wazi kwamba kipofu haoni hata chembe ya mwanga wa dunia hii, japokuwa huwa na hisia kali huenda kuliko mtu anayeona.
Huwa najiuliza swali hili, "hivi kunamtu asiyekuwa mgonjwa lakini anahitaji msaada masaa yote kama kipofu, ukiachilia mbali watoto wadogo?". Tambua kuwa wewe uliye na mboni mbili au moja unauwezo mkubwa sana wa kuweza kujikwamua katika jambo lolote la msingi kimaisha.
Kwaya hii kama umeshawahi kuiiona sehemu yoyote ukiachia mbali siku zile za maonyesho ya kilimo ya nane nane Njiro Arusha inavutia kuisikiliza japokuwa hawaelewi jinsi watu wanavyowaelewa au kuwagusa.Sitakuwa shahidi mimi peke yangu bali watu wengi waliohudhulia maonyesho ya nane nane Arusha waliwazunguka na kuwasikiliza tu.
Ndugu mtanzania mwenzangu tuwasaidie vipofu hapa nchini kwetu hata kwa shilingi mia moja tu, Mungu wa mbinguni atakuongezea, kwasababu huwezi kujua maisha yako ya baadae yatakuwaje. Asanteni na karibuni "asili yetu".

No comments:
KARIBU UTOE MAONI YAKO HAPA