Hifadhi ya Taifa ya Serengeti, yenye ukubwa wa kilomita za mraba 14763, ni Hifadhi ya pili kwa ukubwa nchini (baada ya Hifadhi ya Ruaha). Serengeti ni moja ya Hifadhi maarufu sana duniani. Umaarufu wa Hifadhi hii unatokana na misururu mirefu ya nyumbu wanaohama kwa makundi makubwa kutoka upande mmoja wa mbuga hadi mwingine, na kuvuka mpaka wa Tanzania hadi hifadhi ya wanyama pori ya Maasai Mara nchini Kenya. Wakichagizwa na mvua, kila mwaka zaidi nyumbu milioni moja, pundamilia 2, 00,000, swala tomi 300,000 huunga msafara wa kutafuta malisho na maji.
Hifadhi ya Serengeti, pia ni maarufu kwa wanyama walao nyama chui na samba. Ukubwa wa hifadhi hii umesaidia kudumisha uhai kulinda wanyama walio hatari ya kutoweka kama faru weusi na duma. Katika Hifadhi hii utashuhudia wanyama wawindaji kama duna wanavyowinda.
Aidha zipo aina zaidi ya 500 za ndege. Hifadhi ya Serengeti ipo umbali wa kilomita 335 kutoka Arusha ikiambaa kaskazini katika mpaka wa Kenya na Magharibi inapakana na Ziwa Victoria.Hifadhii inafikika kwa barabara kutokae Arusha, Musoma, au Mwanza na vilevile kwa ndege za kukodi kutoka Dar es salaam, Mwanza, Kilimanjaro, Arusha, Ziwa Manyara, na Ngorongoro.
Wakati mzuri wa kutembelea Hifadhi kuona uhamaji wa nyumbu ni kuanzia Desemba hadi Julai; kuona wanyama wanaowinda Juni – Octoba. Kuna maeneo ya malazi ndani ya hifadhi yenye hadhi tofautitofauti kama Hotel za kitalii, kambi za kifahari, nyumba za wageni, hosteli ya wanafunzi na kambi kadhaa za kupiga mahema ndani ya Hifadhi. Hotel zingine na kambi za mahema hupatikana nje ya Hifadhi.
Viboko hawa ni kivutio kikubwa kwa watalii ndani ya Hifadhi ya Serengeti





No comments:
KARIBU UTOE MAONI YAKO HAPA