Header Ads

Breaking News
recent

WIMBO WA JUSTIN BIEBER "BABY" WALALAMIKIWA NA MTUNZI WA "GOD BLESS THE USA"

All rights reserved to Asili Yetu.


JUSTIN BIEBER NA LEE GREENWOOB (MTUNZI WA WIMBO WA "GOD BLESS THE USA")
 
Kinara wa wimbo wa "Baby" Justin Bieber amelalamikiwa na mtunzi wa wimbo wa "God Bless The USA" bwana "Lee Greenwood" badaada ya kupata taarifa kuwa wimbo wake alioutunga miaka ya 80 ambao umekuwa ukitumika kuimbwa katika matukio maalum ya shule ya  Edna Cohen iliyoko Brooklyn, umebadilishwa na kutumika wimbo wa "Baby" wa Justin Bieber.

Hata hivo principle wa shule hiyo Greta Hawkins ambaye ndiye aliyeubadili wimbo huo wa "God Bless The USA" na kuweka wimbo wa "Baby" (Justin Bieber), alieleza kuwa wimbo huo haukidhi mahitaji kwa watoto wa shule kwasababu unabagua tamaduni za nchi mbali mbali ambazo zimeleta watoto wao katika shule hiyo.

Hata hivyo bwana Lee alimlalamikia principle huyo huku akisema "inakuaje wimbo wangu wa "God Bless The USA" ambao unazungumzia matumaini, imani, upendo na roho uweni wimbo unaowabagua watu wa tamaduni nyingine?". "Nilitunga wimbo huu kwa mapenzi ya nchi yangu na jinsi tulivyo pambana hadi sasa tuko huru".

Na kwa upande wa wazazi wa wanafunzi hao nao walilalamika kama ifuatavyo; "watu wengi wamekuwa wakipambana kuja kuishi huru Marekani, hivyo wimbo huo unapaswa uimbe kwa kiburi chote"alisema mama Luz Lozada ambaye ni mama wa Daniel ambae pia ni mwanafunzi wa shile hiyo.

Msala woote huo ni baada ya wimbo wa Justin Bieber "Baby" kuimbwa katika maafari ya shule hiyo.

No comments:

KARIBU UTOE MAONI YAKO HAPA

Powered by Blogger.