All rights reserved to Asili Yetu.
Nchini China kumekuwa na wimbi la matukio ya kuripuka simu za mikononi huku yakitokea katika sehemu za vituo vya mafuta.Chanzo kimoja kimeeleza kuwa tukio la hivi karibuni limetokea katika kituo cha mafuta ambapo kijana mmoja alikuwa akijaza mafuta kwenye gari yake huku akiongea na simu, wakati akiinama kuchungulia tenki la mafuta ili kujua kama limejaa, mvuke wa mafuta ulikutana na joto kutoka katika simu yake na kusababishamripuko mkubwa.
Hata hivo matukio hayo hayatokei china tu bali Indoneshia, India, Ulaya na kwingineko duniani.Serikali ya China Imepiga mafuku utumiaji wa simu za mkononi katika vituo vya mafuta kwani simu ni kifaa ambacho ukiongea kwa muda hutengeneza joto ambalo likikutana na chemical ya aina yoyote husababisha cheche ambazo husababisha mripuko.
Chanzo hicho kilizidi kueleza kuwa makampuni kama Ericsson, Motorola, Nokia yamekuwa yakitoa maelekezo ya onyo katika vitabu/makaratasi ya maelezo ya jinsi ya kutumia simu.
Hivyo ni vyema kuwa mwangalifu kuongea na simu katika vituo vya mafuta au kuongea na simu wakati ukiwa umeunganiasha kwenye chaji.Kwa maelezo zaidi soma vitabu / makaratasi ya maelezo uliyonunulia simu yako, kama hayapo ni vyema ukamdai muuzaji wa simu.


No comments:
KARIBU UTOE MAONI YAKO HAPA