All rights reserved to Asili Yetu.
JAY- Z
Boss wa Rock Nation Jay- Z anakabiliwa na mashitaka ya kutumia sehemu ya maandishi ya siyo yake katika kitabu chake cha "Decoded" kilichoachiwa mwaka 2010. Patrick White ambaye ndiye mlalamikaji ameeleza kuwa mnamo mwaka 2009 aliibiwa Laptop(kompyuta) yake akiwa na nyaraka zake za maandishi ambazo zimekuja kuonekana katika katika kitabu cha "Decoded" cha msanii Jay- Z.
Patriki aliendelea kufunguka kuwa "kitabu hiki cha 'Decoded' kinamaelezo/rangi/misemo iliyosawa na kazi yangu iliyopotea" na baada ya hapo niliwasiliana na mwandishi msaidizi wa kitabu hicho lakini sikujibiwa.
Patrick alijaza fomu za mahakama ya wilaya kwaajili ya kumshitaki Jay- Z kwa kutumia kazi yake ya maandishi bila ridhaa yake.
"Decoded" pia ni wimbo wa kitabu wa Jay- z huku katika ukurasa mmoja wa kitabu umefafanua kuwa wimbo wa Jay -z wa "99 Problems" ulichangia na kisa cha yeye kukataa kuwaruhusu maaskari kuipekua gari yake.

No comments:
KARIBU UTOE MAONI YAKO HAPA