Header Ads

Breaking News
recent

50 CENT AMENUSURIKA KIFO BAADA YA KUSAIDIWA NA GARI YAKE YENYE UWEZO WA KUZUIA RISASI.

All rights reserved to Asili Yetu.


 50 Cent afunguka baada ya siku chache kupata ajali katika gari yake katika sehemu ya Long Island huko Marekani. Kiongozi huyo wa G - Unit amefunguka katika kituo cha MTV kukanusha uvumi ambao umekuwa ukenezwa na mitandao kuwa amefariki katika ajali ya gari. 50 amesema siku ya ajali alikuwa akiendesha katika upande usiokuwa wake, huku akijaribu kukwepa police ndipo ghafla alipopoteza muelekeo na kujikuta akiigonga Lori iliyokuwa mbele yao."Tungeweza kubanwa sana kama ingekuwa ni gari ya kawaida, ila gari yangu ina vifaa vya ziada vya kuweza kuzuia risasi sawa na vile vya gari analotembelea Rais Obama."

50 Cent aliulizwa kuhusiana na uvumi kuwa ajali hiyo ilikuwa ni ya mikogo au ya vituko tu kabla ya album yake ya "5 (murder by numbers)" kuachiwa. 50 cent alijibu " niamini, mimi nina pesa yakutosha, siwezi kupoteza muda kujigongesha kwenye Lori ili nipate vijipesa kidogo.

No comments:

KARIBU UTOE MAONI YAKO HAPA

Powered by Blogger.