All rights reserved to Asili Yetu.
![]() |
Hapa ni wakati wa makabidhiano ya piki piki. |
Mchungaji wa kanisa la Menonnite Morotonga mkoani Mara Wilayani Serengeti EMANUEL MWIHAGANI amekabidhiwa piki piki aina ya TOYO yenye thamani ya takribani shilingi 1570,000/= iliyonunuliwa na waumini wa kanisa hilo, ili kurahisisha huduma ya injiri katika maeneo mbali mbali ya vijijini. Akitoa shukurani za dhati Mchungaji Emmanuel Mwihagani ambaye ndiye aliyepewa msaada huo, "alisema amani na kupanuka kwa kanisa kunategemea sa na kiongozi wa kanisa, lakini kama itamuwia vigumu kiongozi huyo kinyenzo basi hata kanisa litayumba". Pia aliwashukuru kamati iliyoendesha mchango huo mpaka kufanikisha adhima yao ya kununua piki piki mpya.
Mchungaji huyo aliwaasa pia waumini wa kanisa hilo, kujikita katika shughuli halali za kufanya kazi zitakazo waletea mafanikio katika maisha yao, huku wakimtanguliza Mungu katika mambo yote.
![]() |
Hii ndiyo piki piki iliyonunuliwa kwa michango ya waumini wa kanisa la Menonnite Morotonga Wilayani Serengeti, huku ikigharimu takribani sh. 1570,000 pesa za kitanzania. |
![]() |
Hapa ni picha ya pamoja ya waumini baada ya kumkabidhi mchungaji Emmanuel usafiri wa piki piki. |