VITUKO NDANI YA BASI ZA MIKOANI.
All rights reserved to Asili Yetu.
![]() |
Jana nikiwa safarini, kuliibuka mjadala mzito sana ndani ya basi moja la kwenda mikoani. Mjadala huo ulianza baada ya kuwa bwana mmoja alipopigiwa simu na jirani yake na kumtaarifu kuwa "unataarifa kuwa mwanao alidumbukia ndani ya maji jana saa kumi?" Jamaa kwakuwa ndani ya basi kulikuwa na kelele kidogo ilibidi aongee kwa nguvu kitu ambacho kiliwafanya watu wote waelekeze masikio yote kwake.
Jamaa "Sina taarifa zozote kuhusiana na tatizo hilo, mke wangu hakuniambia chochote, na shangaa anashindwaje kuniambia tatizo kubwa kiasi hicho!". Jirani alidai mtoto yuko hospitali na anaendelea vizuri. Mjadala ulianzia hapo baada ya dada mmoja kuongea kwa hisia kali ya sauti ya juu, huku akipinga kitendo hicho cha jirani kumuelezea yule baba wa mtoto "nimmbea hakupaswa kumwambia huyu bwana". Je ni sahihi kwa kirani mkumpasha habari yule bwana kuhusiana na tatizo lililotokea nyumbani?. Je jirani hakupaswa kufanya hivyo? Changia maoni yako hapo chini...

No comments:
KARIBU UTOE MAONI YAKO HAPA