Header Ads

Breaking News
recent

PICHA ZA HARUSI HUHITAJI MAANDALIZI YAFUATAYO.

All rights reserved to Asili Yetu.

Siku ya harusi inaweza kuwa ni siku ngumu na yenye kuwatia wasiwasi Bwana na Bibi harusi kuonekana tofauti na walivyotegemea. Hizi ni baadhi ya njia pekee zitakazo kusaidia kuondoa wasi wasi na kuonekana katika muonekano mzuri katika siku ya harusi yako.

  1. Kuwa mstari wa mbele katika kufanikisha matarajio yako. Muandae mapema mpiga picha/video wako ili ajue jinsi na aina ya picha utakazohitaji kufotolewa siku ya harusi, na hii itamsaidia kujiandaa na kujua maeneo mazuri ya kuweza kuchukua picha hizo ukumbini. 
  2. Kufotoa baadhi ya picha kabla ya harusi. Hii itakusaidia kupata picha nzuri zitakazo kuwa kumbu kumbu nzuri maishani mwako.Pia hii itamsaidia mpiga picha wako kuchukua picha muhimu nazenye ubora pia.
  3. Panga muda maalum wa kupiga picha.Ili kuokoa muda wakati wa kupiga picha, nivyema kwa pande zote mbili kupiga picha za pamoja kwa pande mbili tofauti, yani upande wa bwana harusi na bibi harusi kabla ya saa za harusi kuanza.
  4. Ielewe mipaka ya kuchukua picha/video katika eneo husika.Nivyema ukapata kibali na maelekezo ya kuchukua picha/video siku ya harusi.Sehemu nyingine kama makanisa, misikiti au mahekaru hawaruhusu kufotoa picha/video ya aina yoyote katika baadhi ya maeneo yao.
  5. Fanya mazoezi ya make-up na kutengeneza nywele.Siku ya harusi sii siku ya kujaribu aina mbali mbali za make-up na mitindo ya nywele, hivyo ni vyema ukatengeneza mitindo mingi ya nywele na make-up, ili upate mtindo mmoja utakao kuonyesha katika muonekano mzuri.
  6. Waandae wasaidizi wako wa harusi.Nivyema ukapanga mapema muonekano sahihi wa sendekeleja wako ikiwa ni pamoja na kuwafanyia make-up mapema.Kufanya hivyo kutasaidia kupendezesha harusi yako.
  7. Jaribu kuchukua muda mfupi muhimu, siku ya harusi kuchukua picha zenu wawili.Kufanya hivyo mtajiwekea kumbu kumbu nzuri katika album yenu ya picha.
  8. Kuwa huru, tabasam na furahi.Maharusi wanao chukuliwa picha nzuri ni wale wenye furaha, tabasamu na wenyekujiachia bila kujali mwanga wa kamera.Siku hiyo ni muhimu na yenye furaha kupata mume au mke mpya.Furahia siku yako wewe pamoja na marafiki, ndugu na jamaa.Mungu akubariki.

No comments:

KARIBU UTOE MAONI YAKO HAPA

Powered by Blogger.