All rights reserved to Asili Yetu.
 |
| Mratibu wa Tanzania Gemological Center Arusha bw.Musa Shanyangi akitufafanulia baadhi ya mashine zinazotumika kuchongea madini na mapambo. |
Akizungumza na
Asili Yetu blog leo mchana ofisini kwake, mratibu wa kitengo cha
'Tanzania Gemological Center' kanda ya kaskazini
Musa Shanyangi, amesema mradi huo unahusika na ukataji madini pamoja na kuchonga mapambo mbali mbali kwa kutumia mawe yanayowekwa nakshi nakshi adimu hapa nchini.
Shanyangi ameeleza kuwa uchongwaji wa mapambo hayo ni kivutio kikubwa sii kwa watarii peke yao bali hata wananchi watavutiwa kununua bidhaa hizo adimu zinazotumika kama mapambo ya ndani.Mratibu huyo ameeleza kuwa mara baada ya kufungua uuzwaji wa vinyago hivyo itawapa fursa wananchi kupata bidhaa hizo kwa bei nafuu ya kitanzania.
Wizara ya nishati na madini kitengo cha madini kanda ya kaskazini kimeanzisha mradi mkubwa wa kuchonga vinyago au mapambo(cavings) kwa kutumia mawe.
Mbali na mapambo ya ndani, pia wanachonga madini mbali mbali kwaajiri ya vito vya kuvaa kama pete na nakshi nakshi tofauti.Kwa wakazi wa Arusha na wale wanaotembelea Arusha wanaweza kujisogeza katika maonyesho ya bidhaa hizi mwezi April hapa Arusha.
Nichukue nafasi hii pia kumshukuru mratibu wa shughuli hii bw. Musa Shanyangi kwa juhudi zake anazozionyesha katika mradi huo wa uchongaji mapambo.Basi baadhi ya kazi zenyewe ni hizo hapo chini.....
 |
| Mratibu wa mradi wa kuchonga mapambo bw. Musa Shanyangi akiwa akionyesha baadhi ya bidhaa zilizokwisha tengenezwa ofisini kwake. |
 |
| Huyu ni American Eagle aliyetengenezwa kwa kutumia mawe, pembeni pia ni ndege wa mawe. |
 |
| Hawa ni aina mbali mbali wa ndege waliochongwa kwa mawe. |
 |
| Wana faa kwa mapambo ndani ya nyumba, hakika nyumba itaonekana ya kisasa. |
 |
| Huyu ni mmoja wa watengenezaji akiwa katika mchakato kuweka sawa vyombo kwaajiri ya kazi. |
 |
| The Arusha Internationa Mem Jewelry And Minerals Fair. |
 |
| Machota wa Asili Yetu blog (kwanyuma) akipewa mchanganuo wa vyombo vya kuchongea vinyago na mratibu wa mradi huo Musa Shanyangi.(wa mbele) |
 |
| Mratibu akionyesha mashine ya kuterezesha bidhaa zinazochongwa hapo. |
 |
| Mmoja kati ya wafanyakazi akichonga madini |
 |
| Ndege huyu amechongwa pia kwa mawe. |
 |
| Hapa akionyesha mashine ya kukelreza. |
 |
| Kikombe kilichotengenezwa kwa mawe. |
No comments:
KARIBU UTOE MAONI YAKO HAPA