Utafiti uliofanywa na wataalamu wa Marekani umebaini
kuwa wanawake wanaoishi kwa matumaini hupunguza uwezekano wa maradhi ya
moyo.
| Matumaini ni Dawa ya moyo |
Utafiti wa hivi karibuni wa watafiti wa Marekani unakariri utafiti wa
awali uliofanywa na kundi la wataalamu wa Uholanzi ukionyesha kupungua
kwa uwezekano wa hatari ya magonjwa ya moyo kwa wanaume.
Utafiti uliofanywa kwa kutumia wanawake laki
moja,ulichapishwa katika jarida la kisayansi, uligundua kuwa watu
wanaoishi kwa hofu walipatikana kua na shinikizo la damu pamoja na
kolestroli au kupungua kwa njia za damu katika mishipa.
Pamoja na hayo hisia za mtu kama tabia ya chuki
kwa wengine pia yanabadili hali ya afya.
Wanawake wenye matarajio mema wana asili mia 9%
ya kupatwa na magonjwa ya moyo na asili mia 14% ya kuuawa kwa magonjwa
yenye uhusiano wa maradhi ya moyo.
Wanawake wa aina hiyo walilinganishwa na wengine
ambao huishi kwa kinyongo, chuki na kijicho kwa wenzao kimawazo au kwa
ujumla kuwashuku wenzao. Hawa wana asili mia 16% kufariki katika kipindi
kifupi kuliko wanaoishi kwa matumaini makubwa ya kufanikiwa.
Uwezekano mkubwa uliopo ni kwamba mtu anayeishi
kwa matumaini huwa na uwezo wa kukabiliana na mitihani ya kimaisha,
mfano wa kukidhi mahitaji yao wanapoumwa.
Utafiti huu ulionelea kuwa wanawake wanaofanya
mazowezi mara nyingi walikuwa wembamba kuliko wenzao wanaoishi na
kinyongo.
Mchunguzi mkuu Dr Hilary Tindle, naibu profesa
wa dawa katika Chuo kikuu cha Pittsburgh, alisema kua ushahidi mwingi
tulioupata unaonyesha kua muendelezo kwa kiwango kikubwa cha fikra za
kutojiamini ni hatari kwa afya."
Msemaji wa shirika la Uingereza ''British Heart
Foundation alisema kua: "tunafahamu kuwa chuki na unyonge husababisha
kemikali fulani mwilini ambazo zinaweza kuzidisha uwezekano wa maradhi
ya moyo, ingawa hatuelewi kikamilifu ni kwanini.
Matumaini au hata chuki ni hisia zinazoweza
kuambatanishwa na tabia zinazokubaliana na afya njema, uvutaji sigara au
chakula kibovu ambavyo vyote vinaweza kuchangia katika afya ya moyo.
"habari njema kwa wanawake ni kua mbali na sura
yako, chaguo lako katika maisha mfano wa chakula au kutovuta sigara kuna
athari kwa moyo usiokua na matatizo kuliko kua na uso mrembo.
Bado kuna hitajika uchunguzi zaidi kujifunza
sababu hisia za aina hii huathiri afya.
Na: BBC
No comments:
KARIBU UTOE MAONI YAKO HAPA