Twitter waongeza idadi ya kuandika maneno katika mtandao huo
Twitter imetangaza kwamba imeanza
kuwafungulia watu wanaoutumia mtandao huo wa kijamii uwezo wa kuandika
ujumbe kwa kutumia tarakimu 280 badala ya 140.
Lakini sasa wamesema watu wengi wataruhusiwa kuandika ujumbe mrefu.
Watakaozuiwa pekee ni wale wanaoandika ujumbe kwa Kijapani, Kichina na Kikorea ambao wanaweza kuwasilisha maelezo zaidi kwa kutumia tarakimu chache.
Twitter wamesema majaribio yalifanikiwa.
Mabadiliko hayo ni sehemu ya mpango wa Twitter kuwavutia watu zaidi.
Mtandao huo kwa sasa una watu milioni 330, idadi ambayo ni ya chini ukilinganisha na milioni 800 wa Instagram na zaidi ya bilioni 2 wa Facebook.
PAKUA NYIMBO ZILIZOTOKA WIKI HII>>>DOWNLOAD
SUBSCRIBE YouTube account yetu upate video zaidi.
Kupata Update kibao, like Facebook account yetu.
Twitter Account yetu>>>Asili Yetu Tanzania
No comments:
KARIBU UTOE MAONI YAKO HAPA