Utafiti: Mbu na Nzi huona kwa haraka zaidi ya binadamu, sababu ziko hapa
Umewahi kujaribu kumuua mbu au nzi?
Utagundua kwamba huwa vigumu sana. Wadudu hawa huwa na kasi ajabu.
Lakini inakuwaje wadudu hawa wadogo - wenye ubongo mdogo hivi - wanaweza
kuwazidi binadamu kwa urahisi hivi?
Ni swali ambalo watu wengi wamekuwa wakijiuliza, lakini usishangae tena.
Sababu ya wadudu hawa kuwazidi binadamu na wanyama wengine ni mtazamo wao wa dunia.
Wadudu hawa huitazama dunia kwa mwendopole yaani slowmotion ukilinganisha na tunavyoyatazama matukio.
Kwa kufafanua, hebu utazame mshale wa saa.
Kama binadamu, huwa unauona mshale huo wa saa ukisonga kwa kasi fulani.
Lakini kwa wanyama wengine hali ni tofauti.
Mfano kasa atautazama ukisonga kwa kasi mara mbili zaidi ya kasi anayoiona binadamu.
Kwa mbu, nzi na wadudu wengine wa karibu, mshale huo wa saa watauona ukisonga kwa kasi mara nne chini ya kasi anayoitazama binadamu.
Kimsingi, kasi ya kusonga kwa wakati hubadilika kutoka kwa mnyama hadi mwingine.
Wanyama kimsingi huutazama ulimwengu kama video inayocheza mfululizo.
Kwa kufafanua, huwa wanaunganisha picha nyingi kutoka kwenye sehemu zao nyingi kwenye macho hadi kwenye ubongo kwa kasi ya juu, mara kadha kila sekunde.
Kwa binadamu, picha hizi hutumwa mara 60 kila sekunde, kwa kasa mara 15 kila sekunde, na kwa mbu, nzi na wadudu wengine wanaopaa mara 250 kila sekunde.
Tofauti
Kasi ambayo picha hizi husomwa kwenye ubongo wa mnyama huweza kupimwa. Kwa kawaida, wanyama wadogo huwa na kiwango cha juu cha kasi hii, ikiwa ni pamoja na mbu na nzi.Binadamu kwa sababu ni wanyama wakubwa, kiwango chao cha kasi hii kiko chini.
Vipimo vyake vimebaini kwamba nzi wenye uwezo wa kuona kwa kasi zaidi wanaweza kutenganisha mng'ao wa mwanga mara 400 kwa sekunde.
Uwezo wao ni mara sita zaidi ya uwezo wa binadamu.
Nzi mwenye uwezo wa juu zaidi hufahamika kama "nzi muuaji". Ni nzi mdogo sana mla wadudu ambaye hupatikana maeneo ya Ulaya.
Huwa anapaa na kuwanasa nzi wengine wakiwa angani kwa kasi ya juu ajabu.
Chanzo: BBC
SUBSCRIBE YouTube account yetu upate video zaidi.

No comments:
KARIBU UTOE MAONI YAKO HAPA