Wasanii Ariana Grande, Rihanna, Taylor Swift na wengineo waguswa na mauaji ya Las Vegas
Staa wa ngoma ya 'Dangerous Women' Ariana Grande ameonekana kuguswa na tukio la shambulio la watu lililotokea Jumapili, October 1 Las Vegas nchini Marekani, ambapo imesemekana kuwa watu takribani 58 wamepoteza maisha na wengine zaidi ya 500 kujeruhiwa.
Shambulio hilo linakuja ikiwa ni baada ya miezi minne tangu tukio la bomu litokee wakati wa tamasha la msanii Ariana Grande huko Manchester, Uingereza, ambapo watu 22 walisemekana kupoteza maisha huku 250 kujeruhiwa.
Ariana amefunguka haya leo kupitia ukurasa wake wa Tweeter>>> "My heart is breaking for Las Vegas," Grande, 24, tweeted on Monday, October 2. "We need love, unity, peace, gun control & for people to look at this & call this what it is = terrorism."
Mastaa wengine walioguswa na tukio hilo na kuandika katika kurasa zao za Tweeter ni pamoja na wasanii wa muziki wa country, Luke Bryan na Carrie Underwood, na wasanii wengine kutoka Vegas, kama vile Mariah Carey na Celine Dion,wengine ni Rihanna, Taylor Swift na wengineo.
SUBSCRIBE YouTube account yetu upate video zaidi.
No comments:
KARIBU UTOE MAONI YAKO HAPA