Header Ads

Breaking News
recent

Fahamu Kiatu ghali zaidi duniani

Bado wanaojua thamani ya vipaji vyao wanazidi kuvitumia kuingiza pesa mfululizo bila hata kumeza fundo la mate. Karibu katika nyumba ya ubunifu Asili Yetu Blog.

Stori zinatoka Dubai kwa mbunifu Debbie Wingham, 35, aliyebuni kiatu ghali sana kuwahi kutokea duniani. 
Debbie Wingham akiwa ameshikilia kiatu ghali zaidi duniani alichokibuni yeye
Kwa mujibu wa ripoti iliyotolewa na watu wa masuala ya mitindo imeeleza kuwa kiatu hicho kinagharibu kaisi cha dola milioni 15.1 za Kimarekani na kimetengenezwa kwa vito mbalimbali kama vile almasi ya blue, almasi nyeupe na vito vingine 1,000 vya almasi.

Kiatu hicho kilichotengenezwa na mbunifu Debbie Wingham aliyopo nchini Dubai, kitakuwa  kitu cha nne chenye thamani kubwa duniani.

Ikumbukwe kwamba mwanamama huyu mnamo 2012 alitengeneza vazi ghali zaidi duniani kwa kutumia almasi yeusi, na mwaka 2013 na 2015 pia aliendelea kutoa vitu ghali zaidi duniani. 

Kwa mujibu wa chanzo Novemba 1, Wingham ataviachia rasmi hivi viatu ghali zaidi duniani huko Raffles Dubai


PAKUA NYIMBO ZILIZOTOKA WIKI HII>>>DOWNLOAD
SUBSCRIBE YouTube account yetu upate video zaidi.

Kupata Update kibao, like Facebook account yetu.
Twitter Account yetu>>>Asili Yetu Tanzania
    

No comments:

KARIBU UTOE MAONI YAKO HAPA

Powered by Blogger.