Watafiti wabaini kuwa Mbwa Mwitu hufanya maamuzi kwa kutumia chafya
Mbwa mwitu hufanya maamuzi yao kwa kupiga kura kupitia kupiga chafya kwa mujibu wa utafiti mpya.
Waligundua kuwa mbwa walitumia chafya kuamua wakati wanaelekea kuwinda baada ya kufanya mikutano inayofahamika kuwa mikutano ya kijamii.
Awali ilikuwa ikifikiriwa kuwa mbwa hao ambao ni familia ya wanyama walio kwenye hatari zaidi ya kuangamia duniani, walikuwa wakipiga chafya ya kawaida.
Lakini wakati watafiti wakirekodi mikutano 68 ya mbwa mwitu waligundua kuwa, wakati walipiga chafya zaidi walikuwa wakiondoka na kuanza kuwinda.
Dr King anasema kuwa chafya hiyo ni lazima ifike kiwango fulani kabla ya wao kuamua kufanya kitu.
Pia utafiti huo uligundua baadhi ya chafya huwa na uzito kuliko zingine.
Stori na BBC
Endelea kufuatilia dondoo kibao za KITOFAUTI duniani kupitia blog yetu ya ASILI YETU TANZANIA. Pia subscribe You Tube account yetu kupata update kibao.


No comments:
KARIBU UTOE MAONI YAKO HAPA