Header Ads

Breaking News
recent

Wapenzi walioachana siku nyingi 'Aishwarya Rai Bachchan' na 'Salman Khan' kucheza filamu moja?

Moja kati ya good moment ambayo haijawahi kutokea kwa miaka mingi ni hii ya mastaa wa filamu kutoka India, hapa namzungumzia mwanadada Aishwarya Rai Bachchan na mkali Salman Khan kukutana katika filamu moja yani uso kwa uso. 

Anyways huenda bado hujang'amua stori ikowapi, basi ni hivi muandaaji wa filamu kutoka Bollywood maarufu kama Sanjay Leela Bhansali inasemekana ametaka kuwakutanisha mwanadada Aishwarya Rai Bachchan na mkali Salman Khan katika filamu inayokwenda kwa jina la Padmavati
Lakini stori inakuja kwamba wakali hawa wali wameshawahi kuwa wapenzi kipindi cha nyuma na kufikia kumwagana na kila mmoja kufanya mambo yake, yani kuanzisha mahusiano mapya, sasa vipi wataridhia kucheza filamu moja?

Stori zimeenea kwa wingi katika vyombo vya habari nchini humo, huku mashabiki wengi wakisubilia kuona hiyo combination kama itafanikiwa. 

Haya sasa kwa upande wa mwanadada Aisharya Rai Bhachchan yeye amekubali ila kwa sharti moja tu, asipangiwe scene moja na mkali Salman Khan

Filamu hiyo iliyokaa kwenye headlines kwa muda sasa inatarajiwa kuachiwa mwezi November 17, huku kwa upande wa Salman Khan akichomoa kuigiza na x-wake katika filamu moja.
Je nini kitakachoendelea? endelea kufuatilia dondoo kibao za mastaa duniani kupitia blog yetu ya ASILI YETU TANZANIA. Pia subscribe You Tube account yetu  kupata update kibao.

No comments:

KARIBU UTOE MAONI YAKO HAPA

Powered by Blogger.