Msanii Ruby afunguka kuhusu Nandy.
Mwanamuziki Ruby aliyefanya poa na ngoma ya 'Na Yule' amewataka
mashabiki zake wasijichanganye kwa kumfananisha na Mwanamuziki 'Nandy'
anayetamba sasa na ngoma 'Wasikudanganye' kwa kuwa kamwe msanii huyo
hawezi kufanya vitu ambavyo yeye anafanya.
"Siwezi kutoa nyimbo mfululizo lakini nitoe ahadi sitaweza kukaa kimya tena .
Chanzo: Eatv
"Nandy
ni msanii wa kike ambaye ni chipukizi amenikuta kwenye game mimi ni
msanii mkubwa sana kwake, kwa Vitu anavyovifanya mimi ninauwezo wa
kufanya zaidi yake. Watu wakisema kwamba ameniacha mbali kimuziki
watakuwa wanakosea kwani mimi ni wa kwanza kuliona jua kabla yake," Ruby amefunguka
Pamoja na kufananishwa aina ya uimbaji wao Ruby ameongeza kwamba "
Nandy nimeshawahi kukutana naye mara chache na niseme hawezi kuimba
kama mimi. Ila mimi Ruby nina uwezo wa kuimba kama yeye na labda siku
moja ninaweza kuimba kama anavyofanya Nandy ili watu wasitufananishe
tena".
Chanzo: Eatv

No comments:
KARIBU UTOE MAONI YAKO HAPA