Mambo 10 ya kushangaza kuhusu watu wanaotumia mkono wa kushoto.
Watu wengi duniani hutumia mkono wa
kulia kwa shughuli nyingi na si ajabu kwamba vitu vingi huundwa kwa
kuwafikiria wanaotumia mkono wa kulia.
Wanaotumia mkono wa kushoto husumbuka sana katika kutumia vitu kama vile mkasi, vitabu au hata kufungua milango.
Fikiria pia kuhusu kipanya katika vituo vya kupokea huduma ya mtandao, mara nyingi utapata kimewekwa upande wa kulia.
Kuna pia viti vyenye sehemu ya kuandikia vyuoni, ni vichache sana hujengwa kwa matumizi ya watu wanaotumia mkono wa kushoto.
Siku ya watu wanaotumia mkono wa kushoto huadhimishwa kila mwaka tarehe 13 Agosti.
Siku hii iliadhimishwa mara ya kwanza mwaka 1976.
Haya hapa ni baadhi ya mambo kumi ya kushangaza kuhusu watu wanaotumia mkono wa kushoto:
1. Asilimia
kumi kati ya watu wote duniani hutumia mkono wa kushoto, na kiwango
hiki kimesalia hivyo kwa muda mrefu. Wanaume wana uwezekano mkubwa wa
kuwa wanatumia mkono wa kushoto.
2. Kwa muda mrefu katika jamii
nyingi, watu wenye kutumia mkono wa kushoto walichukuliwa kuwa dhaifu.
Si ajabu kwamba huenda uliwaona au unawaona watoto wanaochapwa sana kwa
kutumia mkono wa kushoto wakila au wakiandika. Katika baadhi ya jamii,
kutumia mkono wa kushoto huhusishwa na uchawi.
3. Kumsalimia mtu
kwa kutumia mkono wa kushoto kumekuwa kukitazamwa kama kumkosea mtu
heshima. Hii ni kwa sababu watu zamani walikuwa wakitumia mkono wa
kushoto kujitakasa baada ya kwenda msalani.
4. Bingwa wa tenisi
duniani Rafael Nadal alibadilisha na kuanza kutumia mkono wake wa
kushoto akicheza - kutokana na imani ya mkufunzi wake Toni Nadal kwamba
ingempatia nafuu kiasi akikabiliana na wachezaji wengine uwanjani.
5. Mrengo
wa kushoto? Jina hili lilianza kutumiwa miaka ya 1790 baada ya
mapinduzi ya Ufaransa na kuondolewa kwa utawala wa kifalme.
Wawakilishi
wa chama cha kishoshialisto katika bunge walikuwa wakikaa upande wa
kushoto wa kiongozi wa vikao.
Wat wa mrengo wa kushoto wakati huo
walikuwa wakitazamwa kama maadui wa wasomi na watawala.
6. Kwa muda
mrefu, dini ya Kikristo ilihusisha upande wa kushoto na maovu.
Kwenye
picha nyingi za Siku ya Kiama, wale waovu (mbuzi) hutumwa upande wa
kushoto nao wale wa kuokolewa (kondoo) hutumwa upande wa kulia.
Wakati
wa kusulubiwa kwa Yesu, mwizi aliyetubu alikuwa amewekwa upande wa kulia
na yule mwovu alikuwa upande wa kushoto.
7.Watano kati ya marais
wanane wa karibuni zaidi nchini Marekani hutumia mkono wa kushoto
kuandika.
Marais hao ni Gerald Ford, Ronald Reagan, George H.W. Bush,
Bill Clinton, na Barack Obama.
8. Kuna pahala penye jina Left Hand
(Mkono wa Kushoto).
Eneo hilo hupatikana katika jimbo la West Virginia
na hutokana na kijito cha Lefthand Run.
Chanzo: BBC

No comments:
KARIBU UTOE MAONI YAKO HAPA