Aamir Khnan ahamasisha watu kujitolea kuwasaidia watu walioathiriwa na mafuriko Gujarat India
Hali ya maeneo ya Gujarat nchini
India sio nzuri, ikiwa ni baada ya hivi karibuni kukumbwa na mafuriko
makubwa, yaliyosababisha kupoteza maisha ya takribani watu 120 na hasara mbali mbali.
Pamoja na mafuriko ya hivi karibuni yaliyotokea, serikali imekuwa na hasara kubwa. Superstar Aamir Khan amechukua time kupitia ukurasa wake wa Twitter kuonesha huzuni yake juu ya kupoteza maisha na makazi ya watu.
Katika video aliyoiweka Twitter Aamir ameonekana akiwahamasisha watu
kuchukua hatua ya kuwasaidia wakazi wa Gujarat ambao takribani 10,000
kutoka maeneo ya vijijini na mijini wamekosa sehemu ya kuishi.
Aamir anajulikana kwa huduma zake za kijamii na kuwakumbusha watu wajibu wao, kwa wananchi wenzake.
Katika siku za nyuma pia, amewahi kujitoa kuhamasisha watu kujitoa katika kuisaidia jamii.
Hii pia ni hatua muhimu sana iliyochukuliwa na Aamir ili kuwasaidia watu wa Gujarat.
Hii pia ni hatua muhimu sana iliyochukuliwa na Aamir ili kuwasaidia watu wa Gujarat.
No comments:
KARIBU UTOE MAONI YAKO HAPA