Baba yake Beyonce, Mathew athibitisha kuzaliwa kwa watoto mapacha wa mastaa Jayz na Beyonce.
Baada
ya kusambaa kwa tetesi za Beyonce na Jay Z kupata mapacha.
Baba
mzazi wa Queen Bey ambaye pia aliwahi kuwa meneja wake, Mathew Knowles
amethibitisha hilo.
Jumapili hii Knowles aliweka picha ya kadi kwenye mtandao wa Twitter akipongeza kuzaliwa kwa mapacha
hao na kuandika, “They’re here! #beyonce #twins #jayz #happybirthday.”
Katika
kuthibitisha jambo hilo ni kweli, baba huyo wa msanii Beyonce aliweka picha hiyo hiyo
kwenye mtandao wa Instagram na mama yake Beyonce aliweza ku-like picha
hiyo.
Kwa mujibu wa TMZ, inadai kuwa watoto hao wamezaliwa Jumatatu
iliyopita ya Juni 12 lakini mpaka sasa bado wapo hospitalini
hawajaruhusiwa wakiwa chini ya uangalizi pamoja na mama yao.
Blue Ivy Carter ni mtoto (binti) yao wa kwanza, toka wanandoa hao wenye nguvu zaidi duniani kufunga ndoa mnamo mwaka 2008, na kumkaribisha binti yao wa kwanza aitwae Blue mwezi January 7, 2012.
No comments:
KARIBU UTOE MAONI YAKO HAPA