Msichana kati ya waliotekwa na Boko Haram akataa kurudi nyumbani baada ya kuachiliwa huru.
Mmoja
wa wasichana wa Chibok waliotekwa na wapiganaji wa Boko Haram nchini
Nigeria ameamua kusalia na mumewe badala ya kuachiliwa huru kulingana na
msemaji wa rais wa Nigeria.
Garba Shehu aliambia runinga moja kwamba wasichana 83 walitarajiwa kuachiliwa huru lakini mmoja wao akasema : hapana nafurahi nilipo, nimepata mume.
Wapganaji hao wanadaiwa kuwazuilia zaidi ya wasichana 100 kati ya 276 waliowateka katika eneo la Chibok miaka mitatu iliopita.
Chanzo: BBC
No comments:
KARIBU UTOE MAONI YAKO HAPA