Utafiti: Wanawake kula vyakula vya wanga nyakati za usiku mnene, huongeza hatari ya kupata ugonjwa wa kansa.
Wanasayansi kutoka Chuo Kikuu cha Hong Kong wametoa ripoti ya utafiti kuhusu uhusiano uliyopo kati ya kansa ya matiti na kula vyakula vyenye wanga nyakati za usiku ambapo mkuu wa utafiti huo Shelly Tse Lap-ah aliiambia South China Morning Post kuwa, wanawake wanaokula vyakula vyenye wanga kwa wingi kuanzia saa nne usiku wako hatarini kupata kansa ya matiti.
Ripoti hiyo imeeleza kuwa kula vyakula vya wanga nyakati za usiku mnene husababisha kupungua kwa uzalishwaji wa kemikali ya Melatonin
ambayo husaidia kuzuia magonjwa hatari na kuvirahisishia vijidudu
vinavyosababisha kansa ya matiti kushambulia mwili kwa haraka zaidi.
Utafiti
huo uliwahusisha wanawake 1,800 ambapo asilimia 1.76 waligundilika kuwa
na kansa ya matiti iliyosababishwa na kula vyakula vya wanga.
“Kula vyakula vyenye wanga au
Carbohydrate nyingi usiku kunasababisha kuongezeka uzito na magonjwa
kama kisukari.
Mtu akipata magonjwa haya ni rahisi kupata kansa hasa
kansa ya Ini, Tezi Dume na saratani ya matiti.
Utafiti huu umeonesha
kuwa wanawake wanaokula Tambi au Noodles wameathirika zaidi na saratani
ya matiti ukilinganisha na wanawake wanaokula Mchele.” – Dr Francis Chow.
Chanzo: Millardayo
No comments:
KARIBU UTOE MAONI YAKO HAPA