Nyumba ya msanii Nicki Minaj yavamiwa na kuporwa vito vya thamani nchini Marekani.
Polisi kwenye jimbo la Los Angeles
nchini Marekani wanachunguza wizi uliofanyika kwenye nyumba ya Nicki
Minaj amabapo mali ya thamani ya dola 175,000 iliibiwa.
Inaripotiwa kuwa nyumba hiyo ilivunjwa wakati wa uvamizi huo na baadhi ya nguo za Nicki Minaj kuibiwa.
Fanicha iliharibiwa huku picha na chupa za manukato zilivunjwa.
Bado haijulikani ni vipi waalifu waliingia nyumbani humo.
Waliiba vito vya thamani na bidhaa zingine zenye gharama ya dola 175,000.
Source:BBC
No comments:
KARIBU UTOE MAONI YAKO HAPA