Bob Marley baada ya miaka 40, nyimbo zake zapatikana.
Nyimbo zilizokuwa zimepotea za
mwanamuziki Bob Marley, ambazo zilipatikana kwenye chumba cha chini cha
hoteli mjini London baada ya zaidi ya miaka 40 zimetengenezwa upya tena.
Kanda hizo ni za nyimbo za No Woman No Cry, Jamming na Exodus.
Kwaza zilidhaniwa kuharibiwa kabisa kutokana na unyevu uliokuwa eneo kanda hizo zilipopatikana.
Marley ambaye aliaga dunia mwaka 1981, angekuwa na umri wa miaka 72 hii leo.
Kanda hizo zilipatikana kwenye hoteli ya Kensal Rise, kaskazini magharibi mwa London, ambapo Bob Marley na bendi yake walikuwa wakiishi, wakifanya tamasha zao barani Ulaya miaka ya sabini.
Kanda hizo ni kutoka kwa tamasha zilizofanyika maeneo la Lyceum mjini London mwaka 1975, la Hammersmith Odeon 1976, na la Rainbow mjini London mwaka 1977.
Source: BBC
No comments:
KARIBU UTOE MAONI YAKO HAPA