Sayansi Na Teknolojia: Usawa wa bahari huenda ukainuka kwa zaidi ya mita 6.
Utafiti mpya uliotolewa kwenye gazeti la sayansi la Marekani unaonesha
kuwa, joto la maji ya sehemu ya juu baharini linafanana na lile la
kipindi cha mwisho kati ya enzi mbili za barafu, lakini katika kipindi
hiki usawa wa bahari ulikuwa juu kuliko sasa kwa mita 6 hadi 9.
Watafiti kutoka Chuo Kikuu cha Oregon cha Marekani wameonesha wasiwasi kuhusu mwelekeo wa ongezeko la joto duniani.
Watafiti kutoka Chuo Kikuu cha Oregon cha Marekani wameonesha wasiwasi kuhusu mwelekeo wa ongezeko la joto duniani.
Kipindi cha mwisho kati ya enzi mbili za barafu kilikuwa katika miaka laki 1.29 hadi laki 1.16 iliyopita, ambacho ni kimoja kati ya vipindi vyenye joto kubwa zaidi kabla ya binadamu kutokea duniani.
Watafiti wamechambua sampuli za
miamba zilizokusanywa kutoka sehemu 83 chini ya bahari, na kugundua
kuwa joto la maji ya juu ya baharini kuanzia mwaka 1870 hadi mwaka 1889
karibu liwe sawa na lile la mwanzoni mwa kipindi cha mwisho kati ya enzi
mbili za barafu, na joto la maji kuanzia mwaka 1995 hadi mwaka 2014 ni
karibu sawa na joto kali zaidi kwenye kipindi hiki.
Prof. Andrew Watson wa Chuo Kikuu cha Essex cha Uingereza amesema, usawa wa bahari utabadilika kutokana na kuongezeka kwa joto duniani, lakini mchakato huo unaendelea polepole, huenda unahitaji maelfu ya miaka.
Profesa huyu
alisema habari nzuri ni kwamba watu bado wana muda wa kubadili mwelekeo
huo kwa kupunguza utoaji wa hewa zinazosababisha kuongezeka kwa joto, na
habari mbaya ni kwamba miji ya pwani itazama baharini katika miaka
mingi ijayo.
Credit:CRI
No comments:
KARIBU UTOE MAONI YAKO HAPA