Mafua ya ndege tahadhari yatolewa.
Baada ya ugonjwa wa mafua ya ndege kugundulika nchi jirani
ya Uganda baada ya kuwepo kwa vifo vingi vya ndege pori katika maeneo ya Lutembe beach, Masaka, Kachanga, Bukibanga
na Bukakata na vifo hivyo kutokea kwa baadhi ya ndege wafugwao (kuku na bata)
na inahisiwa kuwa ndege hao wamepata virusi vya ugonjwa huo kutoka kwa ndege
pori wanaohama kutoka nchi za Ulaya.
Baada ya taarifa hizo Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii,
Jinsia, Wazee na Watoto leo January 18 2017 imetoa taarifa kuhusu kuwepo kwa
virusi vya mafua makali ya ndege katika nchi jirani ya Uganda. Aidha taarifa hiyo imeeleza kuwa maeneo
yalioathirika ni maeneo yanayozunguka ziwa Victoria pamoja na ziwa lenyewe.
Taarifa iliyotolewa na wizara ya afya imesema kuwa hadi sasa
hakuna binadamu yeyote aliyeonekana kuwa na dalili za ugonjwa huo huko nchini
Uganda hivyo wametoa tahadhari kuwa kuna uwezekano mkubwa wa ugonjwa kusambaa kwa
binadamu ikiwa hatua madhubuti za
kujikinga hazitazingatiwa.
Taarifa ya wizara imetaja haya ya kuzingatia ili kudhibiti
kuenea kwa ugonjwa huo.
*Kutoa taarifa
endapo wataona kutokea kwa vifo vya
ndege pori au wafugwao (kuku, bata na wengineo) kwa wataalamu wa mifugo, afya
au ofisi ya serikali iliyo karibu nawe-:
* Kutokugusa mizoga
au ndege wagonjwa bila kutumia vifaa kinga
* Kuepukana na tabia
ya kuishi nyumba moja na ndege wafugwao
* Kuepuka kuchinja
kuku au bata wanaoonyesha dalili yoyote ya ugonjwa
* Kunawa mikono
vizuri kwa kutumia sabuni
* Kupika nyama au
mayai ya ndege kwa muda mrefu usiopungua nusu saa. .
* Kuepuka kushika
ndege wa porini na ndege wa majumbani wanaohisiwa kuwa na ugonjwa huu.
Source: Millard Ayo
No comments:
KARIBU UTOE MAONI YAKO HAPA