Wanawake watajwa kuwa na maambukizi zaidi ya VVU nchini.
Tanzania imeadhimisha siku ya Ukimwi duniani kwa kuzindua bodi na mfuko
maalum wa ukusanyaji wa rasilimali za mapambano dhidi ya UKIMWI ambapo
inakadiriwa kuwa watu zaidi ya milioni moja na laki tano wanaishi na
virusi vya Ukimwi nchini.
Akizungumza na waandishi wa habari Jijini
Dar es Salaam, Waziri wa Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu,
Jenista Mhagama katika siku ya maadhimisho hayo hulenga kuwakumbuka
wahanga wa janga la Ukimwi pamoja na mapambano dhidi ya ugonjwa huo
amesema maambukizi ya ukimwi Tanzania bara ni asilimia 5.3 ambapo
wanawake wameonekana wakiongoza katika kupata maambukizi hayo
ukilinganisha na wanaume.
Aidha Muhagama alisema takwimu zilizopo sasa zinaonyesha kuwa
asilimia 6.2 ya wanawake wameambukizwa ugonjwa wa Ukimwi ikilinganisha
na asilimia 3.8 ya wanaume.
“Sasa kuathirika kwa wanawake na janga hili ni asilimia 6.2 ambapo
wanaume ni asilimia 3.8 lakini vilevile inakadiriwa kuwa kuna watu
takribani 1,538,882 wanaoishi na VVU katika nchi yetu ya Tanzania,”
alisema Muhagama.
Hata hivyo Waziri Muhagama aliweza kutoa ufafanuzi juu ya mfuko
unaozinduliwa alisema umepitishwa na sheria ya Bunge namba 6 ya mwaka
2015 lengo likiwa ni kukusanya mapato ya ndani ya wenye virusi vya
Ukimwi.
“Kila Mtanzania ana wajibu wa kuokoa maisha yake na maisha ya
mwenzake kuhakikisha anakuwa ni sehemu ya kukusanya rasimali za mfuko
huu ili kupambana na tatizo la ukimwi katika nchi yetu ya Tanzania,”
alisema.
BY: EMMY MWAIPOPOSource Bongo5
No comments:
KARIBU UTOE MAONI YAKO HAPA