Ripoti ya Shirika la Afya duniani kuhusu ugonjwa wa moyo Afrika.
Ripoti mpya za shirika la Afya Duniani
(WHO) zinasema kuwa ugonjwa wa shinikizo la damu ndio ugonjwa ambao
unaathiri watu wengi zaidi barani Afrika huku ikionesha asilimia zaidi
ya 10 ya Waafrika wameshapata na ugonjwa huo.
Kwa
mujibu ripoti hiyo imeeleza sababu kubwa za kuzidi kuongezeka kwa
ugonjwa huo kuwa ni watu kupuuza kufanya mazoezi, kupunguza au kutotumia
kabisa matunda angalau matano na mboga kwa siku, matumizi ya tumbaku au
sigara na pombe zimetajwa kama njia kuu za kushindwa kupambana na yote
yasiyoambukiza ikiwemo Moyo, Kisukari na Kansa.
Ripoti ya
Shirika la Afya Duniani (WHO), imeonesha pia robo ya watu wazima kutoka
nusu ya nchi za Afrika zilizofanyiwa utafiti wameathiriwa na sababu tatu
za hatari zinazoongeza uwezekano wa kuwa na moja au zaidi ya magonjwa
mengine hatarishi wakati wa maisha yao.
WHO inaonyesha kuwa wanawake wa Afrika wenye umri wa zaidi ya miaka 45 wako katika hatari zaidi ya kuambukizwa magonjwa haya.
Wakati
ambapo matumizi ya tumbaku au sigara na pombe yako kiwango cha chini
barani Afrika kuliko sehemu zingine duniani, shinikizo la damu
liko katika kiwango cha juu zaidi duniani, na kuathiri karibu nusu ya ya
watu wazima barani Afrika.
Kwa
mujibu wa WHO, kiwango hicho kinatisha kwa sababu ugonjwa huo unaathiri
pole pole na mara nyingi unagunduliwa baada ya miaka kadhaa ukiwa
umeshafanya madhara makubwa kwa mgonjwa. Pia ripoti hiyo imeonesha kuwa
bara la Afrika ni sehemu pekee watu wanakabiliwa na utapiamlo na fetma.
WHO imeeleza kuwa matatizo haya yanaweza kuzuiwa kwa watu kula vizuri, kunywa kwa kiasi na kufanya mazoezi na endapo tahadhari
hizi hazizingatiwi, hali hii inaweza kupelekea kuzigharimu serikali
mabilioni ya pesa kwenye matibabu ya wagonjwa wake.
Source: millardayo.com
No comments:
KARIBU UTOE MAONI YAKO HAPA