Meli inayofanana na ile ya Titanic kutengenezwa na China.
Titanic ni moya meli kubwa sana duniani iliyoweka historia toka inatengenezwa mnamo April 2, 1912 ikiwa imebuniwa na mbunifu aitwae Thomas Andrews.
Mashua sawia na iliyotengenezwa
katika mji mkuu wa Belfast huko Ireland ya Titanic itawekwa katika eneo
la kumbukumbu la theme park nchini India.
Ujenzi huo wa mashua
hiyo yenye urefu wa kina cha mita 269, itawekwa katika hifadhi iliyoko
mashambani , katika mkoa wa Sichuan.
Ujenzi huo uliaza siku ya Alhamisi.
Mashua
ya Titanic iliyojengwa na Harland na Wolff huko Belfast , iligonga
mwamba wa barafu na kuzama Kaskazini mwa Atlantic mwaka 1912 hatua
iliyosababisha vifo vya zaidi ya watu 1,500.
Mashua hiyo ilikuwa katika safari yake kutoka Southampton ikielekea New York.
Habari kuhusu meli hiyo ni swala ambalo liliwashangaza raia wengi kutoka China.
Hisia
zaidi ziliibuka mwaka 1997, baada ya filamu iliyokuwa ikimuangazia Kate
Winslet na Leonardo DiCaprio, kuwa maarufu nchini humo.
Muelekezi wa
filamu, James Cameron, kutoka Canada, alikuwa na mashua kama hiyo
iliotengezwa kwa maswala ya uigizaji pekee , lakini hakuna mashua sawia
na hiyo iliowahi kutengenezwa.
Bilionea mmoja kutoka Australia,
Clive Palmer, alitangaza mipango yake ya kutengeneza mashua kama ya
Titanic mwaka 2012, lakini mradi huo bado haujakamilika.
Meli hiyo
ya China, itakuwa yenye umbo sawa na ile ya Titanic , itakuwa na sehemu
ya michezo, maonyesho, kuogelea na sehemu maalum ya watu maalum ambayo
itakuwa na mtandao wa Wifi na inatarajiwa kuwa kivutio kikubwa katika
eneo hilo la theme park lililoko kilomita kadhaa kutoka pwani ya China.
Kampuni
hiyo ilitangaza mipango ya mradi huo, utakaogharimu Yuan bilioni moja
mwaka 2014, kulingana na shirika la habari la AF.
Source: BBC
No comments:
KARIBU UTOE MAONI YAKO HAPA