Kumbu kumbu ya kuadhimisha miaka 9 tangu kifo cha msanii maarufu wa Raggae, Lucky Dube.
Leo, Oktoba 18, ni miaka 9 tangu mwanamuziki wa nyota wa reggae wa Afrika Kusini, Lucky Dube auawe kwa kupigwa na risasi.
Kwa
heshima ya mwanamuziki huyo, waziri wa sanaa na utamaduni, Nathi
Mthethwa amelitaka taifa hilo lisherehekee mchango wake kwenye muziki.
“Today we pay tribute to Raggae music icon Lucky Dube who died
tragically on this day in 2007. His music touched millions across the
globe,” ameandika kwenye Twitter.
Oktoba 18, 2007, Lucky Dube aliuawa
kwenye kitongoji cha Rosettenville jijini Johannesburg, muda mfupi
baada ya kuwashusha watoto wake wawili kati ya saba kwenye nyumba ya
mjomba wao.
Polisi wanasema watu waliomuua hawakujua kama nini yeye na
walidhani ni Mnaijeria. Watu watano walikamatwa na watatu walipatikana
na hatia na kuhukumiwa March 31 2009.
Wawili kati yao walijaribu kutoroka na walikamatwa. Walihukumiwa kifungo cha maisha jela.
Source: Bongo5
Source: Bongo5


No comments:
KARIBU UTOE MAONI YAKO HAPA