Faida 10 za kula Matikitimaji na Matango.
Ulaji
wa matango na matikiti maji husaidia kuboresha kiwango cha maji ambayo
huitajika mwilini, hii ni kutokana na matango kuwa na kiwango kikubwa
cha maji ambayo husaidia kuondoa taka mwili pamoja na sumu mbalimbali
ambazo miili yetu huzipata kupitia vyakula, madawa na hata vinywaji.
(1)Husaidia
kupunguza uzito wa mwili. Kutokana na kuwa na asili ya nyuzi nyuzi au,
fibres, humfanya mlaji ajisikie kushiba bila ya kuongeza vitu mwilini
ambavyo husababisha mtu aongezeke uzito hivyo kuzuia magonjwa mbalimbali.
(2)Hupunguza
(hangovers),uchovu, mawengewenge pamoja na hali ya kujisikia vibaya
kutokana na unywaji wa kilevi. Hii ni kutokana na kuwa na vitamini B na
maji mengi ambapo, baada ya mtu kunywa kilevi na kisha akaja kula
matango kabla ya kulala, itamfanya asubuhi asiamke huku akiwa na
hangovers.
(3) Husaidia
katika mmeng'enyo wa chakula, matatizo ya tumbo kama vile kuvimbiwa,
tumbo kujaa gesi, vidonda vya tumbo na mengineyo hupungua kutokana na
ulaji wa matango, husaidia kuondoa sumu tumboni na kurahisisha
ufyonzwaji wa protein mwilini kutokana na uwepo wa kiwezeshaji cha
kibaiolojia kinachoitwa, erepsin enzyme.
(4) Husaidia
kuondoa msongo wa mawazo kwani yana kiwango kikubwa cha vitamini B
ambayo husaidia kuboresha utendaji kazi wa mishipa mbalimbali ya fahamu
mwilini na hivyo kuondoa hatari ya mtu kuathirika na msongo wa mawazo
unaosababishwa na maisha ya kila siku.
(5) Husaidia kuondoa hatari ya mtu kupata kansa. Yana kiwango kikubwa cha virutubisho vyenye asili ya mimea viitwavyo, lignans, ambavyo pamoja na vitamini c.
(6) husaidia kuondoa sumu mbalimbali na kuiboresha kinga ya mwili na hivyo kuepusha hatari ya mtu kupata kansa.
(7) Husaidia
kuondoa harufu mbaya kinywani. Kwa kukiweka kipande cha tango mdomoni
kwa dakika kadhaa, huuwa bakteria mbalimbali wasababishao magonjwa
mbalimbali ya kinywa na harufu mbaya mdomoni..
(8) Husaidia mtu kupata choo laini na huzuia kukosa choo.
(
9) Huzuia
kuganda kwa mafuta katika mishipa ya damu ili kuwezesha mzunguko sahihi
wa damu kaitika pande zote za mwili sambamba na kurekebisha mapigo ya
moyo.
(10) Huwepo wa vitamini katika matunda haya husaidia kupunguza kiwango cha sukari mwilini na presha.
Source: Mo Blog


No comments:
KARIBU UTOE MAONI YAKO HAPA