NIMEKUWEKEA HAPA STORY ZOTE ZA KIPINDI CHA "ZIG ZAG HOT STORIES" YA JANA JANUARY 23 KUTOKA 95.7 IDEA FM RADIO.
Kama ulikosa wakwetu kusikiliza kipindi kitamu cha ZIG ZAG HOT STORIES kinacho angazia Story Hot Duniani, utazipata 95.7 IDEA FM RADIO ARUSHA kinachoruka Juma Tatu hadi Ijumaa saa Moja jioni hadi saa nne usiku, basi story zilizo husika ziko hapa.....
1. Taarifa sio
nzuri kutoka Saudi Arabia, vyombo vikubwa vya habari kama CNN, Sky News na BBC vinaripoti kuhusu msiba wa aliyekuwa Mfalme
wa Saudi
Arabia, Abdullah
Bin Abdulaziz ambaye amefariki akiwa Hospitalini akipatiwa matibabu.
2. Mwanamke Vera Jaber
amejifungua wakati akiwa kwenye ndege iliyotoka Jordan kuelekea New York, wahudumu wa ndege walitoa
msaada kwa mama huyo kujifungua na kundelea na safari hadi walipofika New York
ambako mwanamke huyo na mtoto wake walipelekwa Hospitali.
3. Video ya
wimbo mpya wa Bebe Cool, Everywhere I Go
kutoka kwenye album yake ya,Go Mama Album 2015. Video imeongozwa na God Productions.
4. Ile video ya
hip hop iliyokuwa ikisubiliwa sana nchini Uganda hatimae imekwisha dondoka
machoni mwa mashabiki wa muziki Afrika Mashariki. Wimbo huo wa video unaokwenda
kwa jina la ‘NEW
DAY’ ni wa msanii Atlas Da African ft. Lilian Mbabazi, huku Director wa video hiyo akiwa ni Sasha Vybes.
5. Mshindi wa Big brother Africa 2014 Idris Sultan
ambae anaendeleza matunda ya ushindi wake wa BBA na sasa kajipatia nyumba yake
ya kuishi ambayo pamoja na mengine ina sebule mbili na anatarajia kuanza kuishi kwenye
nyumba hiyo kuanzia Jumapili January
25 2015.
6. Mratibu wa
shirika la kijamii Chiwute alisema, utafiti ulionesha kuwa,wasichana na
Wanawake milioni
100 hadi milioni 140 ulimwenguni wanaishi na machungu au
madhara yanayotokana na ukeketaji huku waathirika walio wengi wakiwa ni Kati ya umri wa miaka 15.
7. Mwanamke
mwenye umri wa miaka
90 nchini Kenya ambaye
anahudhuria masomo akiwa na wajukuu zake wapatao sita inaaminika ndiye mwanafunzi
mzee zaidi Duniani anayesoma Shule ya msingi.
8. Wema
amekanusha vikali kuhusu habari zilizoenea kuwa amempeleka Diamond Platnumz polisi kutokana na
deni la milioni
10 alilokuwa akimdai.
Usikose WAKWETU kufuatilia kipindi hiki kinacho kukusanyia mengi yanayotokea katika mitandao ya habari kote duniani na WAKWENU CHOTA BOY.
No comments:
KARIBU UTOE MAONI YAKO HAPA