ALBUM YA MSANII 'ANGEL BENARD IKO TAYARI. MP3
ANGEL BENARD ni jina ambalo
limekuwa likisikika kwa miaka kadhaa sasa kwenye ulimwengu wa muziki wa
gospel. Angel Benard mwenye miaka 25 hatimaye sasa anaachia album yake
NEW DAY kwenye mfumo wa digitali kupitia Mkito.com. Watu wengi
wamekuwa wakisubiri kusikia nyimbo zake za zamani lakini haikuwa rahisi
kuzipata. Album hii ni album ya 3 ya mwana dada huyu mwenye sauti ya
maajabu. Ni wasanii wachache sana wa muziki wa gospel ambao wamefanikiwa
kuvusha nyimbo zao zikapendwa na wapenzi wa gospel pamoja na wapenzi wa
muziki wa bongo flava, RnB n.k. na mwimbaji huyu ni mmoja wapo.
Katika
kuitambulisha album hii Angel Benard ataachia wimbo mmoja kila siku ya
Alhamis kwa wiki 10 mfululizo. Wimbo wa kwanza utatoka tarehe 23 October
na unaitwa NEED YOU TO REIGN ukiwa katika miondoko ya Reggae.

No comments:
KARIBU UTOE MAONI YAKO HAPA