MABADILIKO YA MBIO ZA SOKOINE MINI MARATHON 2014.
![]() |
| Washiriki wa Sokoine Mini Marathon - Monduli 2013. |
Tunaomba radhi kwa kufanya mabadiliko ya ghafla! Hiyo ni
kutokana na mashauriano kati yetu sisi waandaaji, Chama Cha Riadha Mkoa na wanariadha wenyewe.
SABABU KUU: Imeamuliwa kwamba siyo vizuri kuwakimbiza
wanariadha mbio ndefu mara mbili kwa wiki moja sababu pia kutakuwa na
Ngorongoro Half Marathon April 19, 2014.
Familia imeridhia ombi letu na pia imekuwa wazo zuri kwa
wanariadha wazoefu ambao wanafahamu athari za kukimbia mbio ndefu mfululizo.
Pia wananchi wengi sasa wataweza kushiriki Kilomita 10.
Taratibu zingine hadi sasa zipo kama ilivyopangwa, ila namba
zinasajiliwa katika uwanja wa Sheikh Amri Abeid Karume. Tsh: 2,000 tu kwa
kusajili namba yako. ZAWADI ZITATOLEWA KWA WASHINDI.
Source: www.gidabuday.blogspot.com
Source: www.gidabuday.blogspot.com

No comments:
KARIBU UTOE MAONI YAKO HAPA