HER MOTHER'S DAUGHTER (Episode ya 71 & 72) CELYN ATEKWA NA KUFANYIWA UNYAMA.
![]() |
Ameigiza kama "Mio" jambazi au baba yake Diego. |
Baada ya baba yake Diego kutoa vitisho vingi kwa Theresa na Lucas huku akimtumia Diego katika kuperereza mambo, sasa wachukua hatua nzito na kufanikiwa kumteka Celyn. Margaux na Liam walijitahidi sana kumuokoa Celyn katika mikono ya Diego na baba yake lakini juhudi ziligonga mwamba. Ethan naye alijitosa lakini aliambulia kupigwa risasi mkononi.
Baba yake Diego nampa Lucas masharti kuwa asipotoa milioni 20 hatomuachia Celyn na atatoboa siri zote alizonazo kuhusu maovu yote ya Lucas. Lucas kusikia hivyo anaingiwa na uoga na kukubaliana na sharti hilo. Walimfunga Celyn kamba na kumpa kichapo kweli.
Kabla ya kupelekewa pesa baba yake Diego na Diego mwenyewe walikaa kibarazani wakipata kinywaji, hukondani Celyn akigugumia maumivu makali, alivuta glasi ya maji kwa mguu na kuivunja, alifanikiwa kuitumia kukata kamba na kutoka nje. Pale nje alibakia baba yake Diego, alikuwa amelewa na kusinzia.
Celyn alinyata na kwenda mpaka pale mezani na kufanikiwa kuchukuwa simu na kumpigia Liam. Celyn alijitahidi kukimbia kwani pia Liam na Ethan walimfuta alipowaelekeza. Diego aliporudi alikuta Celyn hayupo na kuamua kuwasha gari kumsaka.
Ghafla Celyn aliona gari inakuja, aliisimamisha akiomba msaada, kumbe alikuwa Diego, alimpakia kwa nguvu na kumrudisha alikokuwa ametekwa.
Siku ya siku iliwadia Lucas kupeleka pesa kwa baba yake diego ili amuachie Celyn, lakini Beatrice aliseti askari endapo chochote kitatokea basi mashambulizi yachukue nafasi. Kabla ya yote, baba yake Diego alimkabidhi Diego kitabu cha ulithi kilichokuwa kimesheheni siri ya uovu wa Lucas.
Maaskali walizunguka eneo zima la makabidhiano, lakini masharti ilikuwa ni Theresa ndiye alitakiwa kuzipeleka zile pesa. Theresa alichukuwa begi huku watu wote wakiwa wanamtazama kwenye camera zilizokuwa zimetegeshwa hapo. Jambazi alimuamulu Diego amlete Celyn. Lakini kumbe Lucas bado alikuwa na wasi wasi kuwa huenda Jambazi akikamatwa atatoboa siri, hivyo aliagiza mtu ampige risasi.
Ghafla jambazi alipigwa risasi, na kudondoka chini, askari waliwasiri na Diego alitoroka na Celyn akiwa na begi la pesa. Alipoona amezidiwa aliamua kufyatua risasi na moto mkubwa kuwaka. Alifanikiwa kutoroka na pesa na kumuacha Celyn akiwa ameangukiwa na chuma mguuni.
Moto ulizidi kuwa mkubwa huku maaskari wakiwazuia Liam na Margaux wasiingie kumtafuta Celyn kwani walidhani bado atakuwa na Diego, lakini Margaux alitumia nguvu na kufanikiwa kumkuta Celyn akiwa amebanwa na chuma. Kwa bahati nzuri Liam naye alifika na kumbeba Celyn.
Ethan yeye alikuwa upande wapili wa lile jengo, ghafla alimuona Diego akiwa ameshikilia begi, alimfuata na kuanza kumfukuza. Alipomfikia walipigana na Ethan kuonekana kumdhibiti Diego hadi maaskari walipofika na Diego kufanikiwa kujitupa katika daraja refu na kudhaniwa amefariki.
DONDOO ZIJAZO:
Baba yake Diego aliwahishwa hospitali na Lucas kwa kushinikizwa na Diego amefanikiwa kumtorosha hospitali, je nini kitatokea? Fuatili Thamthilia hii hapa ASILI YETU TZ.