"HER MOTHER'S DAUGHTER" (Episode ya 68) CELYN MSICHANA MREMBO AJITOA MUHANGA KWAAJILI YA BABA YAKE.
![]() |
| Celyn |
Baada ya Julio kupigwa risasi na baba yake Joshua yani Diego, baada ya kujua kuwa Ethan ameanza kung'amua jambo pamoja na picha ya baba yake kutapakaa kwa baadhi ya wana ndugu wa Julio. Alichofanya Diego baada ya kuingia nyumbani kwa Theresa, aliiba picha ya baba yake iliyokuwa katika mkoba na kutokomea nayo.
Diego amekuwa akijishtukia kila anapoulizwa kuhusu kama anamtambua mtu aliyempiga Julio risasi, kitu kinachoonyesha kabisa anamfahamu mlenga shabaha. Diego anawahi nyumbani kwake na kumtorosha baba yake, lakini wakati akimtorosha kwa gari yake yenye rangi nyekundu, Ethan alikuwa mahali akimtazama na hivyo kuamua kumpia simu Celyn na kukutana nae kuzungumza jambo hilo.
Celyn na Ethan wakiwa wanateta ghafla Margaux aliingia na kuwakuta wakiteta, lakini mara walipomuona wakanyamaza, kitu ambacho kilimshitua na kwenda hadi kwa Liam na kumwambia kuwa amemuona Celyn na Ethan wakiteta jamba, japokuwa wamekataa kumuambia walichokuwa wakiongea.
Liam anashikwa na wivu na kumzuia Celyn asiendelee kushirikiana na Ethan katika kumfuatilia baba yake Diego, lakini Celyn anagoma na kumhakikishia Liam kuwa atakuwa muangalifu. Bado Margaux naye aliingiwa na wivu na kulazimika kumlazimisha Celyn amuambie. Celyn aliamua kumwambia.
Kumbuka kuwa baba yake Diego alitumwa na Lucas ili akawafanyizie familia ya Theresa, lakini yeye aliamua kumpiga risasi Julio. Lucas alipokutana na mtu huyo alimgombeza na kuwa amekeuka utaratibu wa kazi. Lakini baba yake Diego alikuwa mkali na kuamua kuahidi kumfanyizia Lucas, hata hivyo Lucas naye alikuwa akijiamini sana kwa kuwa na pesa na ulinzi.
Margarux anaamua kumfuata Diego na kumpasulia ukweli wote kuwa Celyn na Ethan wanamfatilia ili kujua ukweli wa jambazi. Margaux anamchukua Diego hadi hospitali alikokuwa Celyn na kutoboa siri mbele ya Diego. Celyn anabaki mdomo wazi, Diego aliamini kuwa tayari alikuwa amekwisha wachonganisha Margaux na Celyn, lakini kumbe laah! Baada ya hapo Margaux na Celyn walikutana na kucheka, kumbe ilikuwa ni mbinu ya kumuingia Diego ili atoboe ukweli mzima.
DONDOO ZIJAZO:
Je upelelezi wa Margaux, Celyn na Ethan utafanikiwa kumtia mbaloni jambazi? Julio ghafla hali yake inazidi kuwa mbaya je atapoteza maisha? Theresa alionekana kumuomba msamaha Beatrice, je amemsamehe?, Jambazi anamtokea Theresa na kuahidi kuwauwa mtu mmoja mmoja katika familia yake, je itakuwaje? Karibu Sana Asili Yetu Tanzania ulete matangazo yako ya biashara na karibu kwa dondoo zijazo.

No comments:
KARIBU UTOE MAONI YAKO HAPA